Rais Dkt John Magufuli akizindua Kituo kidogo cha Polisi kinachohamishika wakati wa uuzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi (Call Centre) katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam. kutoka kulia ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu, Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba, Kaimu MkuruMwakilishi wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva, Mkurugenzi Mkuu wa CRDB, Dk Charles Kimei, Katibu Mkuu kiongozi , John Kijazi na Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida.
Benki ya NMB ndio waliofadhili uzinduzi huo ambapo walitoa kiasi cha sh milioni 143 kwaajili ya kufanikisha uzinduzi wa tukio hilo ikiwa ni pamoja na kutoa vituo viwili vya Polisi vya kuhamishika.
Rais Dkt John Magufuli akizindua Kituo kidogo cha Polisi kinachohamishika wakati wa uuzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi (Call Centre) katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam. Kushoto ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani , Mwigulu Nchemba.
Rais Dkt John Magufuli akipata maelezo katika mabanda mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi (Call Centre) katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Rais Dkt John Magufuli akimkabidhi tuzo ya ufadhili Mkurugenzi Mtendaji w a TBA Bw. Elius Mwakalinga wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo. Kutoka kushoto ni Waziri wa mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba, IGP Ernest Mangu, Katibu Mkuu Kiongozi, John Kijazi, , Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkurugenzi Mkuu wa benki ya CRDB, Dk Charles Kimei.
Rais Dkt John Magufuli akimkabidhi tuzo ya ufadhili Bi. Edna Rajabu wa kwa niaba ya Shirika la Utangazaji la TBC wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo. Kutoka kushoto ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba, IGP Ernest Mangu, Katibu Mkuu Kiongozi, John Kijazi, , Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkurugenzi Mkuu wa benki ya CRDB, Dk Charles Kimei.
Sehemu ya wananchi na wadau waliohudhuria uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo.
Sehemu ya wananchi na maofisa wa benki ya NMB waliohudhuria uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo.
Rais Dkt John Magufuli akihutubia uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo.
Rais Dk John Magufuli akikagua kituo cha mawasiliano ya polisi (Call centre) katika kituo cha Polisi Kati jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi. .Pamoja naye ni Waziri wa mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba (katikati), Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Ndani Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia), IGP Ernest Mangu (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (watatu kushoto) na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
**************
Rais Dk John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Juni, 2016
amezindua kituo cha mawasiliano cha Jeshi la Polisi ambacho kitarahisisha
utoaji wa taarifa za uhalifu na kuharakisha askari polisi kufika katika eneo la
tukio.
Kituo hicho cha
kwanza kuanzishwa na Jeshi la Polisi hapa nchini kipo katika kituo kikuu cha
Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam na
kinafanya kazi kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano ya simu na mfumo wa
utambuzi wa eneo (GPS) ambapo askari polisi waliopo katika kituo cha
mawasiliano watakuwa wakipokea simu kutoka kwa wananchi wanaotoa taarifa za
matukio ya uhalifu na kisha kuwaelekeza askari walio jirani ili wafike eneo la
tukio na kukabiliana na wahalifu.
Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini Inspekta Jenerali (IGP) Ernest Mangu amemueleza Rais Magufuli
kuwa kituo hicho kina uwezo wa kupokea simu 18 kwa mpigo kutoka kwa watu
wanaopiga simu ya bure namba 111 au 112 kwa ajili ya kutoa taarifa za uhalifu
na kwamba lengo la jeshi hilo ni kuhakikisha askari wanafika eneo la tukio
ndani ya dakika 15.
IGP Mangu ameongeza
kuwa kituo hicho kimeanzishwa kwa msaada kutoka benki ya CRDB iliyotoa shilingi
milioni 320, kitaanza kutoa huduma tarehe 01 Julai, 2016 kikianzia katika mkoa
wa Kipolisi wa Kinondoni Kanda maalum ya Dar es salaam na polisi imejiwekea
malengo ya kuwa na vituo kama hivyo nchi nzima ifikapo mwaka 2019.
Akizungumza katika
uzinduzi wa kituo hicho, Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi kwa
kuanzisha mradi huo na ameahidi kuwa serikali itahakikisha inaunga mkono mpango
huo ikiwa ni pamoja na kulifanyia kazi ombi la kununuliwa helkopta itakayorahisisha
zaidi ufikaji eneo la tukio.
Aidha, Rais
Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi kuwanyang’anya silaha wahalifu kabla
hawajawadhuru raia na kupora mali zao ama kusababisha mauaji, na amewataka
viongozi wa jeshi hilo kuwazawadia askari wanaofanya kazi nzuri ya kupambana na
wahalifu.
Dkt. Magufuli pia
ametaka jeshi la polisi lisimame imara kuhakikisha serikali inatekeleza ahadi
zake kwa wananchi zikiwemo upatikanaji wa maji na huduma nyingine za kijamii na
kwamba hatarajii kuona mtu yeyote anafanya vitendo vitakavyosababisha ahadi
hizo kutotekelezwa.
Katika
hatua nyingine, Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh
Aboubakar Zubeir Ali amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli kwa juhudi kubwa anazozifanya katika kuiongoza nchi.
Mufti Mkuu Sheikh
Aboubakar Zubeir Ali ametoa pongezi hizo jana jioni tarehe 24 Juni, 2016 Ikulu
Jijini Dar es salaam katika futari iliyoandaliwa na Rais Magufuli na akatumia
nafasi hiyo kuwasihi Waislamu na watanzania wote kwa ujumla kukataa vitendo
vinavyoashiria uvunjifu wa amani.
“Niwahusie ndugu
zangu watanzania wote, kwamba amani ni kitu muhimu tuitunze amani tuliyokuwa
nayo, tuienzi amani tuliyonayo, na hapo tutakuwa tunaisadia serikali na
tutakuwa tunamsadia Mhe. Rais katika kuilinda amani”
Amesema Mufti Mkuu.
0 comments:
Post a Comment