Nafasi Ya Matangazo

June 25, 2016

Rais  Dkt John Magufuli akizindua Kituo kidogo cha Polisi kinachohamishika wakati wa uuzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi (Call Centre) katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam. kutoka kulia ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu, Waziri wa  Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba, Kaimu MkuruMwakilishi wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva, Mkurugenzi Mkuu wa CRDB, Dk Charles Kimei, Katibu Mkuu kiongozi , John Kijazi na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida. 

Benki ya NMB ndio waliofadhili uzinduzi huo ambapo walitoa kiasi cha sh milioni  143 kwaajili ya kufanikisha uzinduzi wa tukio hilo ikiwa ni pamoja na kutoa vituo viwili vya  Polisi vya kuhamishika. 
Rais Dkt John Magufuli akizindua Kituo kidogo cha Polisi kinachohamishika wakati wa uuzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi (Call Centre) katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam. Kushoto ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani , Mwigulu Nchemba.
Rais  Dkt John Magufuli  akipata maelezo katika mabanda mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi (Call Centre) katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Rais Dkt John Magufuli akimkabidhi tuzo ya ufadhili Mkurugenzi Mtendaji wa TBA Bw. Elius Mwakalinga wakati wa  uzinduzi  wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi  katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo. Kutoka kushoto ni  Waziri wa mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba, IGP Ernest Mangu, Katibu Mkuu Kiongozi, John Kijazi,  , Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkurugenzi Mkuu wa benki ya CRDB, Dk Charles Kimei.
Rais Dkt John Magufuli akimkabidhi tuzo ya ufadhili  Bi. Edna Rajabu wa kwa  niaba ya Shirika la Utangazaji la TBC  wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi  katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo. Kutoka kushoto ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba, IGP Ernest Mangu, Katibu Mkuu Kiongozi, John Kijazi,  , Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkurugenzi Mkuu wa benki ya CRDB, Dk Charles Kimei. 
Sehemu ya wananchi na wadau waliohudhuria uzinduzi  wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi  viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo. 
 Sehemu ya wananchi na maofisa wa benki ya NMB waliohudhuria uzinduzi  wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi  viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo. 
 Rais  Dkt John Magufuli akihutubia  uzinduzi  wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo. 
Rais Dk John Magufuli akikagua kituo cha mawasiliano ya polisi (Call centre) katika kituo cha Polisi Kati jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi. .Pamoja naye ni Waziri wa mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba (katikati), Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Ndani Meja Jenerali Projest  Rwegasira (kulia), IGP Ernest Mangu (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (watatu kushoto) na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.


**************
Rais Dk John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Juni, 2016 amezindua kituo cha mawasiliano cha Jeshi la Polisi ambacho kitarahisisha utoaji wa taarifa za uhalifu na kuharakisha askari polisi kufika katika eneo la tukio.

Kituo hicho cha kwanza kuanzishwa na Jeshi la Polisi hapa nchini kipo katika kituo kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya  Dar es salaam na kinafanya kazi kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano ya simu na mfumo wa utambuzi wa eneo (GPS) ambapo askari polisi waliopo katika kituo cha mawasiliano watakuwa wakipokea simu kutoka kwa wananchi wanaotoa taarifa za matukio ya uhalifu na kisha kuwaelekeza askari walio jirani ili wafike eneo la tukio na kukabiliana na wahalifu.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali (IGP) Ernest Mangu amemueleza Rais Magufuli kuwa kituo hicho kina uwezo wa kupokea simu 18 kwa mpigo kutoka kwa watu wanaopiga simu ya bure namba 111 au 112 kwa ajili ya kutoa taarifa za uhalifu na kwamba lengo la jeshi hilo ni kuhakikisha askari wanafika eneo la tukio ndani ya dakika 15.

IGP Mangu ameongeza kuwa kituo hicho kimeanzishwa kwa msaada kutoka benki ya CRDB iliyotoa shilingi milioni 320, kitaanza kutoa huduma tarehe 01 Julai, 2016 kikianzia katika mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Kanda maalum ya Dar es salaam na polisi imejiwekea malengo ya kuwa na vituo kama hivyo nchi nzima ifikapo mwaka 2019.

Akizungumza katika uzinduzi wa kituo hicho, Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuanzisha mradi huo na ameahidi kuwa serikali itahakikisha inaunga mkono mpango huo ikiwa ni pamoja na kulifanyia kazi ombi la kununuliwa helkopta itakayorahisisha zaidi ufikaji eneo la tukio.

Aidha, Rais Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi kuwanyang’anya silaha wahalifu kabla hawajawadhuru raia na kupora mali zao ama kusababisha mauaji, na amewataka viongozi wa jeshi hilo kuwazawadia askari wanaofanya kazi nzuri ya kupambana na wahalifu.

Dkt. Magufuli pia ametaka jeshi la polisi lisimame imara kuhakikisha serikali inatekeleza ahadi zake kwa wananchi zikiwemo upatikanaji wa maji na huduma nyingine za kijamii na kwamba hatarajii kuona mtu yeyote anafanya vitendo vitakavyosababisha ahadi hizo kutotekelezwa.

Katika hatua nyingine, Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa juhudi kubwa anazozifanya katika kuiongoza nchi.

Mufti Mkuu Sheikh Aboubakar Zubeir Ali ametoa pongezi hizo jana jioni tarehe 24 Juni, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam katika futari iliyoandaliwa na Rais Magufuli na akatumia nafasi hiyo kuwasihi Waislamu na watanzania wote kwa ujumla kukataa vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani.

“Niwahusie ndugu zangu watanzania wote, kwamba amani ni kitu muhimu tuitunze amani tuliyokuwa nayo, tuienzi amani tuliyonayo, na hapo tutakuwa tunaisadia serikali na tutakuwa tunamsadia Mhe. Rais katika kuilinda amani” Amesema Mufti Mkuu.
Posted by MROKI On Saturday, June 25, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo