Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akitembelea na kuzungumza na wananchi wa Kikusya na kuwahakikishia juu ya ujenzi wa barabara ya Kikusya - Matema kukamilika.
Moja ya madaraja yaliyopo katika barabara hiyo ya kikusya - Matema
akiendelea na ziara yake
Mkuu wa mkoa wa Mbeya amewataka wawekezaji na wananchi kujiandaa kutumia BARABARA ya kikusya- Matema Beach kwa ajili ya kukuza biashara na uwekezaji.
Amependezwa na mandhari nzuri ya ziwa Nyasa na anaamini kukamilika kwa barabara hiyo kutaongeza biashara na uwekezaji. Kwa mujibu wa mkataba barabara hii itakamilika 31 Julai 2017
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya amewataka wananchi kutoa ushirikiano na wakala wa barabara Tanroad katika ujenzi wa barabara ya Kikusya- Matema inayojengwa kwa kiwango cha lami
Ameweleza kusikitishwa na tukio la hivi karibuni la wananchi wa kijiji cha Makwale kuwapiga na kuwajeruhi wafanyakazi 15 wanaojenga barabara hiyo kwa kisingizio cha kutoa ajira kwa vijiji vinavyopitiwa na mradi huo
Amewaeleza faida ya barabara hiyo inayogharimu sh bilioni 56.9 kuwa kukamilika kwake itaongeza uwekazaji katika ukanda wa Ziwa Nyasa, urahisishaji was biashara na usafiri wa uhakika wakati wote.
Amewaweka wazi kuwa ameona barabara Nyingi za lami hujengwa kuunganisha Mkoa na mkoa, nchi na nchi na mijini lakini barabara hii ni ndani ya halmashauri inatoka mjini kwenda kijijini mpaka beach hivyo ni muhimu tufike ujenzi wa barabara hii na kutoa ushirikiano
Kuhusu suala la ajira mkandarasi amekubali kuajiri watu 100 kutoka Vijiji vinavyopitiwa na mradi huu.
Aidha amewataka Tanroad kuharakisha uhakiki kwa wananchi wote waliopisha barabara ili walipwe fidia
0 comments:
Post a Comment