Mkurugenzi
Mtendaji wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, John Wanga, akizungumza wakati wa kukabidhi
madawati katika Manispaa hiyo.
Utengenezaji wa Madawati ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, ukiendelea katika karakana ya Shule ya Sekondari ya wavulana Bwiru.
************ ************
Halmashauri ya Manispaa ya
Ilemela mkoani Mwanza, imekabidhi madawati 2,600 kwa shule zote 74 za Msingi za
umma zilizopo kwenye manispaa hiyo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la
Rais Dkt.John Pombe Magufuli la kutaka kila wilaya kumaliza tatizo la madawati
ifikapo Juni 30 mwaka huu.
Madawati hayo ambayo
yametengenezwa kwenye karakana ya shule ya sekondari ya wavulana ya Bwiru, ni
sehemu ya mpango wa kutengeneza madawati 9,080 na hivyo kumaliza kabisa tatizo
la uhaba wa madawati katika manispaa hiyo.
Akikabidhi madawati hayo hii
leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ilemela, John Wanga, amesema madawati
hayo yametengenezwa kutokana na fedha zitokanazo na makusanyo ya ndani pamoja
na michango ya wadau wengine ambapo katika mgawo wa awali, kata zote 19 za
manispaa hiyo zimepewa madawati 139 kila moja.
Wanga amesema kila dawati moja
lenye uwezo wa kukaliwa na wanafunzi watatu, limegharimu shilingi 98,000 ambapo
manispaa ilinunua vifaa ikiwemo mbao, misumari na vyuma na kulipa gharama za
ufundi zinazofikia shilingi 15,000 kwa kila dawati na kwamba madawati mengine
yaliyobakia kukidhi mahitaji yanaendelea kutengenezwa kwenye karakana hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya
ya Ilemela, Manju Msambya, amepiga marufuku matumizi ya madawati hayo kwenye shughuli
nyingine ikiwemo mikutano ya kisiasa huku akiwataka wazazi,walezi na jamii
nzima kwa ujumla kutambua umuhimu wa kuchangia juhudi za kuboresha elimu.
Renatus Mulunga ambae ni
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela amesema halmashauri hiyo inafanya kila
jitihada kuhakikisha kwamba inatatua tatizo la upungufu wa madawati kwa shule
za msingi katika manispaa hiyo, hatua ambayo itasaidia kuboresha ari ya
wanafunzi kujisomea.
Picha Zaidi Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment