Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Hamza Johari (kushoto )akikabidhiwa zawadi na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa China(CAAC), Xu Ho,Mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kuanzisha ushirikiana wa wataalam kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na wataalam kutoka Mamlaka ya China.(CAAC) kiklichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
****************
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), na Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya China (CAAC), zimeanzisha rasmi ushirikiano katika maeneo ya utalaam, ufundi na mafunzo katika nyanja ya Usafiri wa Anga.
Hayo yalibainishwa rasmi jana, baada ya uongozi wa TCAA ukiongozwa na Mkurugenzi wake Mkuu Hamza Johari ulipokutana na ugeni toka China ukiongozwa na Mkurugenzi wake Mkuu wa CAAC Xu Hao, walipokutana Makao Makuu ya TCAA, Ukonga Banana jijini.
Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Johari alisema Tanzania na China zina mkataba ikiwa ni makubaliano muda mrefu katika nyanja ya mafunzo na kubadilishana uzoefu na mafunzo, ila kinachofanyika sasa ni kuanza rasmi kwa utekelezaji wa makubaliano hayo.
Johari alisema, hatua hii itasaidia hasa ukichukulia Tanzania uwezo ni mdogo katika nyanja za utaalam na teknolojia katika miundombinu.
“Lengo ni kuwa na miundombinu ya kisasa lakini kwa gharama nafuu na pia wataalam wetu kuanza kupata mafunzo ya mara kwa mara nchini China”.
Johari aliongeza pia, eneo jingine litakalofaidika katika kuanza rasmi kwa utekelezaji wa makubalino hayo ni eneo la usalama , ambapo sasa wataalam wa usalama wa Anga wa TCAA watapata fursa ya mafunzo nchini china.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Hamza Johari (kushoto) akiongewa wakati wa kikao kilichohusisha wataalam kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na wataalam kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya China(CAAC). Jijini Dar es Salaam leo , Lengo la kikao hicho ni kuanzisha ushirikiano katika maeneo ya utalaam, ufundi na mafunzo katika nyanja ya Usafiri wa Anga. Watatu kutoka kushoto nni Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya usafiri wa Anga Nchini China (CAAC) Xu Ho.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Hamza Johari (kushoto wa tatu ) na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa China(CAAC), Xu Ho (wane kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa mamlaka hizo mbili wakati wa kikao cha kuanzisha ushirikiana wa wataalam kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na wataalam kutoka Mamlaka ya China.(CAAC) kiklichofanyika leo jijini Dar es Salaam
0 comments:
Post a Comment