Nafasi Ya Matangazo

June 18, 2016

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akikabidhi sehemu ya vyakula hivyo kwa Mwenyekiti wa Kituo cha Charambe Islamic Center Dkt. Haruni Kondo aliyepokea kwa niaba ya vikundi vigine vinne. Mke wa Rais amekabidhi mchele kilo 500, sukari kilo 500 na tende kilo 28, tukio hilo limefanyika katika ofisi ya Mke wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akikabidhi sehemu ya vyakula hivyo kwa Mwenyekiti wa Kituo cha Charambe Islamic Center Dkt. Haruni Kondo aliyepokea kwa niaba ya vikundi vigine vinne. Mke wa Rais amekabidhi mchele kilo 500, sukari kilo 500 na tende kilo 28, tukio hilo limefanyika katika ofisi ya Mke wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam.
Khalifa wa Zawiyatul lqadiria, Abas Hamdan watatu kutoka kulia akiongoza dua ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na viongozi wengine wakuu wa serikali mara baada ya tukio la kukabidhi vyakula hivyo. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Mke wa Waziri mkuu Mama Marry Majaliwa pamoja na viongozi mbalimbali vya vikundi vya kulea watoto yatima na watu waishio kwenye mazingira magumu. BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa na  mke wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa vikundi vya kulea watoto yatima na watu waishio kwenye mazingira magumu. Tukio hilo limefanyika katika Ofisi za Mke wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Mama Mlezi wa Kituo cha Charambe Islamic Center Asile Zahali mara baada ya kukamilika zoezi la utoaji wa vyakula mbalimbali kwa vituo vinne vya kulea watoto na watu waishio kwenye mazingira magumu.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa na mke wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa akizungumza na viongozi mbalimbali wa vituo hivyo kabla ya kuwakabidhi vyakula hivyo katika Ofisi yake Ikulu jijini Dar es Salaam.
***********        ***********
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli amekabidhi chakula kwa ajili ya futari wakati huu wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa vituo vinne vya kulea watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu Jijini Dar es salaam.

Vyakula hivyo vimekabidhiwa leo tarehe 18 Juni, 2016 katika ofisi ya Mke wa Rais Ikulu Jijini Dar es salaam vimejumuisha Mchele kilogramu 500, Sukari kilogram 500 na Tende kilogramu 28.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vyakula hivyo, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli aliyeongozana na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa amewatakia heri Waislamu wote katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuwasihi waendelee kuliombea Taifa amani na utulivu.

 (“Tunawatakia mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, katika kipindi hiki tunawaomba mzidi kuiombea nchi yetu amani, viongozi wetu wa nchi na watanzania wote kwa ujumla, nchi ikiwa na amani ndio mambo mengi mazuri yanaweza kufanyika”)

Kwa niaba ya vituo vilivyopatiwa vyakula hivyo, Mwenyekiti wa Kituo cha Charambe Islamic Center Dkt. Haruni Kondo amemshukuru Mke wa Rais kwa kutoa vyakula hivyo na ameeleza kuwa kitendo hicho kinaonesha mshikamano na ushirikiano walionao watanzania wote bila kujali tofauti ya dini, kabila wala maeneo wanayotoka.

 (“Kwa hiyo ndugu zangu mna imani ya kikristo lakini mnatambua waislamu ni ndugu zenu, wote tunajenga nyumba moja, mshikamano ndio tunu tuliyoachiwa na Baba yetu wa Taifa, leo mmeguswa kuona wenzenu tunafanya ibada na nyinyi mmeingia kwenye ibada, sasa ibada ya kutoa ni ibada kubwa sana, sio nchi nyingi katika Afrika zinafanya kitendo hiki, watu hawaelewi, ni nchi chache sana ambazo imani moja inaunga mkono imani nyingine, lakini sisi waislamu tunalitambua hili hata toka kipindi ambacho mtume wetu SWA anapigana kusimika dini hii kwa waumini alipata nusura kwa wakristo”) 

Vituo vilivyokabidhiwa vyakula hivyo ni Charambe Islamic Center, Tasofe Lqadiria, Nur Twarigatu Lqadiria na Zawiyatul Lqadiria.
Posted by MROKI On Saturday, June 18, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo