BENKI ya DCB leo inazindua tawinlake jipya la Benjamin Mkapa lilopo jirani na Ofisi za Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam. Uzinduzi wa tawi hilo ni moja ya jitihada za Benki hiyo za kusogeza huduma zake jirani na wananchi. Mgemi rasmi katika uzinduzo huo ni kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene akikata utepe kuzindua rasmi tawi la 9 la Benki ya DCB hii leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Bank, Edmund Mkwawa akisoma hotuba yake
Manispaa ya Ilala wakipokea gawio lao la sh milioni 132.8
Manispaa ya Temeke wakipokea gawio lao la sh milioni 119.2
Mfuko wa Bima ya Afya nao ni moja ya wanahisa wa DCB Bank nawao walipokea gawio la sh milioni 83.6.
Hotel ya Riki Hill nao walipata gawio la sh Milioni 10.1
Baada ya uzinduzi wa tawi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene aliingia ndani na kusaini kitabu cha wageni.
Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Bank, Edmund Mkwawa akizungumza. Mkwawa aliomba serikali kuangalia upya agizo lake la hivi karibuni kwamba benki za
biashara ziwe zinahamisha fedha za taasisi za serikali na Halmahsauri za
Manispaa kwenda Benki Kuu kwani utekelezaji wa agizo hili utadhoofisha sana
benki yetu na hivyo kuathiri ufanisi wa benki kwa zaidi ya asilimia 40%.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya DCB, Balozi
Paul Rupia alisema kuwa changamoto kubwa inayoikabili benki hiyo ni ukosefu wa
amana za muda mrefu (stable deposits) kukidhi idadi kubwa ya mikopo inayoombwa
na wateja kwa ajili ya kuendeleza biashara zao mbalimbali na kuboresha maisha
yao. Nakuongeza kuwa jitihada za kufuatilia katika ngazi mbalimbali kuomba
Manispaa zitumie benki yao hazikuzaa matunda na kumuomba Waziri kwakuwa Manispaa
hizo ziko chini yake aingile kati suala hilo ili Manispaa za Dar Es Salaam na
Jiji ziweze kutumia benki yao kikamilifu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene akizungumza ambapo katika hotuba yake
alisema kuwa amefurahishwa na benki hiyo kuwa karibu sana na wananchi
wanaowazunguka kwa kutoa jumla ya Tshs. milioni 135 kwa huduma za kijamii na
kwamba mwaka huu mna mpango wa kutoa madawati 300 kwa Manispaa za Ilala,
Kinondoni na Temeke. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Aidha, akiguzia changamoto inayoikabiliBenki
hiyo hususani suala la Manispaa za Dar es Salaam kutumia benki hiyo katika
shughuli zote za kibenki. Ametoa wito kwa wananchi kuona fahari ya kuwa na Benki
inayofanya vizuri kiasi hiki hivyo wafungue akaunti, wakope na wajivunie kuwa na
Benki yao.
“Nawaasa wadau wote katika sekta hii hasa
wanahisa waanzilishi zikiwemo Manispaa za Dar-es-Salaam na Jiji kufungua
akaunti katika benki ya DCB na kutumia huduma mbalimbali zinazotolewa na benki
hii ili kupunguza tatizo la ukosefu wa amana za kudumu,” alisema
Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya DCB Commercial Bank Plc wakiwa katika uzinduzi wa tawi hilo jipya la Benjamin Mkapa lililopo jirani na Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Wanahisa mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo
Wafanyakazi wa Benki ya DCB tawi jipya la Benjamin Mkapa lililopo jirani na ofisi za Jiji la Daes Salaam wakiwa tayari kupokea wageni mbalimbali wanaofika katika uzinduzi huo. Kushoto ni Neema Gabriel na Kulia ni Aneth Lusama.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene akipokea hundi ya sh milioni 39 kwaajili ya kuchangia ununuzi wa madawati jijini Dar es Salaam.
Umoja Unity wakipiokea gawio lao la Sh Milioni 193.9 kutokana na faida. Manispaa ya Ilala wakipokea gawio lao la sh milioni 132.8
Manispaa ya Temeke wakipokea gawio lao la sh milioni 119.2
Mfuko wa Bima ya Afya nao ni moja ya wanahisa wa DCB Bank nawao walipokea gawio la sh milioni 83.6.
Hotel ya Riki Hill nao walipata gawio la sh Milioni 10.1
Baada ya uzinduzi wa tawi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene aliingia ndani na kusaini kitabu cha wageni.
Baada ya uzinduzi wa tawi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene akisaini kufungua akaunti katika benki hiyo.
0 comments:
Post a Comment