BENDI ya muziki ya African Stars “Twanga Pepeta” itazindua albamu yake
ya 13 ijulikanayo kwa jina la Usiyaogope
Maisha mkoani Mwanza kwenye
ukumbi wa Villa Park Jumamosi.
Akuzungumza jijini jana, Mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka alisema
kuwa maandalizi ya uzinduzi huo yamekwisha kamilika na wanamuziki wake wapo
kwenye maandalizi ya mwisho kwa ajili ya uzinduzi huo.
Mbali ya wimbo wa Husiyaogope Maisha uliotungwa na Ali Choki, nyimbo nyingine zinazounda albamu hiyo
ni Ndoa (Luizer Mbutu), Uso Chini, (Choki), Michepuko (Msafiri Diouf), Mapenzi
Yanaumiza (Haji Ramadhani) na Ganda la Mua uliotungwa na Saleh Kupaza ambaye
kwa sasa hayupo kwenye bendi hiyo.
Asha alisema kuwa wamekwisha rekodi nyimbo zote na mauzo ya CD 1000 ya
kwanza, yatatumika kuchangia ununuzi wa madawati mkoani humo. Alisema kila CD
itauzwa Sh3, 000 na Sh 1,000 watatumia kununua madawati.
“Hii ni heshima kwa wapenzi wa muziki wa Mwanza, bendi inafanya
uzinduzi wa albamu hii kwa mara ya kwanza mkoani, albamu zote 12
zilizinduliwa hapa
Dar es Salaam, hii ni mara ya kwanza katika historia ya bendi yetu,”
“Tunataka tuwe tofauti, mpango wa kununua madawati pia utafanyika
katika uzinduzi wa albamu hiyo kwa mkoa wa Dar es Salaam katika siku
itakayopangwa, tumepiga hesabu na kujua dawati moja ni Sh50,000 (kama
utatengeneza mwenyewe), “ alisema Asha.
Alisema kuwa albamu hii ni ya aina yake kwani wanamuziki wake wametunga
nyimbo ambazo mbali ya kuburudisha, pia zinatoa mafundisho mbalimbali.
Albamu za nyuma ya bendi hiyo ni Kisa Cha Mpemba, Jirani, Fainali Uzeeni,
Chuki Binfasi, Ukubwa Jiwe, Mtu Pesa, Safari 2005, Password, Mtaa wa Kwanza, Mwana Dar es Salaam, Dunia
Daraja na Nyumbani ni Nyumbani.
0 comments:
Post a Comment