Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Kayanza Peter Pinda
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa
Mizengo Peter Pinda kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).
Mheshimiwa Mizengo
Peter Pinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Dkt. Asha-Rose Mtengeti
Migiro ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.
Taarifa
iliyotolewa leo tarehe 25 Mei, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi
imeeleza kuwa uteuzi wa Mheshimiwa Pinda unaanza mara moja.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano,
IKULU
Dar es salaam
25 Mei, 2016
0 comments:
Post a Comment