Mwenyekiti wa kampuni ya Gidani akitoa maelezo ya mchezo huo kwa baadhi ya wakazi wa mji wa Dodoma
Mbunge wa zamani jimbo la Nanyumbu Dastan Mkapa (kulia) akipewa maelezo namna mshindi wa bahati nasibu ya Taifa atakavyopatikana mara baada ya kukata tiketi ya mchezo huo katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma jana baada ya kuzinduliwa rasmi ukataji tiketi za mchezo
Mkurugenzi wa Bodi ya michezo ya bahati nasibu ya Taifa ,Abbas Tarimba akiwaelekeza wananchi jinsi mashine za mchezo huo zinavyofanya kazi
Wakala wa ukataji tiketi za mchezo wa bahati nasibu ya Taifa mjini Dodoma Jamila Baduwel akitoa huduma hiyo kwa mmoja wa wananchi aliyetaka kununua tiketi za kushiriki.
************************
BAADA
ya kampuni ya Murhandizwa kutoka nchini Afrika ya Kusini
ambayo ilipewa leseni ya kuendesha mchezo wa bahati nasibu ya taifa kuanza
kuuza tiketi za mchezo huo wiki iliyopita, Jumamosi Mei 28,2016 ndio mchezo wa kwanza
utafanyika na mshindi wa kitita cha shilingi milioni 100 atatangazwa. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Mwenyekiti
wa kampuni ya Gidani International ambayo ni kampuni mama ya kampuni ya
Murhandizwa,Prof .Bhongani Khumalo alisema kuwa michezo yote itaendeshwa kwa
utaalamu kwa kutumia teknolojia ya kisasa na kwa uwazi vilevile kuanza kwa mchezo huo hapa nchini ni mwendelezo wa
michezo mingine mingi ya bahati nasibu itakayokuja baadaye.
“Kampuni
yetu inao uzoefu wa muda mrefu kuendesha michezo ya Bahati Nasibu na
tutahahakikisha watanzania wananufaika
na mchezo huu pia tutachangia pato la taifa kwa njia ya kodi kupitia mchezo
huu.Aliongeza kuwa uchezeshaji
wa mchezo utakuwa wa wazi kupitia vyombo vya habari na mshindi atakuwa
anatangazwa na kupatiwa fedha zake mara moja bila kuwepo urasimu wa aina
yoyote.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubatisha ya Taifa,Abbas
Tarimba aliwataka watanzania kuchangamkia fursa hii kwa kununua tiketi za
kushiriki katika mchezo kutoka kwa mawakala waliosambaa nchini kote ili waweze
kujishindia zawadi ya mamilioni ya fedha na kubadilisha maisha yao.
Tarimba
aliwataka wananchi wasiwe na hofu ya kushiriki kwenye mchezo kwa kuwa
unafanyika kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa na serikali “Wananchi
wasiwe na wasiwasi kushiriki kwenye mchezo huu kwa kuwa fedha zao na kanuni za
uendeshaji wa mchezo vinasimamiwa na serikali.
Alisema
ujio wa mchezo huu nchini mbali na kuwanufaisha washindi binafsi utachangia kupanue wigo wa ajira kwa
Watanzania wengi watakaosimamia zoezi la ukatishaji tiketi katika vituo zaidi
20,000 vitakavyofunguliwa Nchi nzima.
Tiketi
za mchezo huu zimeanza kuuzwa nchi nzima na wakati wa uzinduzi wa huduma za
kampuni mkoani Dodoma wananchi wengi walijitokeza kununua tiketi za kushiriki
na walishauri mtandao wa kuuza tiketi ufanyike kupitia hata kwenye simu za mkononi
ili kuwawezesha wananchi wengi kushiriki kununua tiketi ambayo kila moja
inauzwa shilingi 500/-.
0 comments:
Post a Comment