Nafasi Ya Matangazo

May 27, 2016

 Mwenyekiti wa kampuni ya Gidani akitoa maelezo ya mchezo huo kwa baadhi ya wakazi wa mji wa Dodoma
Mbunge wa zamani jimbo la Nanyumbu Dastan Mkapa (kulia) akipewa maelezo namna mshindi wa bahati nasibu ya Taifa atakavyopatikana mara baada ya kukata tiketi ya mchezo huo katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma jana baada ya kuzinduliwa rasmi ukataji tiketi za mchezo
 Mkurugenzi wa Bodi ya michezo ya bahati nasibu ya Taifa ,Abbas Tarimba akiwaelekeza wananchi jinsi mashine za mchezo huo zinavyofanya kazi
Wakala wa ukataji tiketi za mchezo wa bahati nasibu ya Taifa  mjini Dodoma Jamila Baduwel akitoa huduma hiyo kwa mmoja wa wananchi aliyetaka kununua tiketi za kushiriki.
************************
BAADA ya  kampuni ya Murhandizwa kutoka nchini Afrika ya Kusini ambayo ilipewa leseni ya kuendesha mchezo wa bahati nasibu ya taifa kuanza kuuza tiketi za mchezo huo wiki iliyopita, Jumamosi Mei 28,2016 ndio mchezo wa kwanza utafanyika na mshindi wa kitita cha shilingi milioni 100 atatangazwa. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Mwenyekiti wa kampuni ya Gidani International ambayo ni kampuni mama ya kampuni ya Murhandizwa,Prof .Bhongani Khumalo alisema kuwa michezo yote itaendeshwa kwa utaalamu  kwa kutumia teknolojia ya kisasa na kwa  uwazi vilevile  kuanza kwa mchezo huo hapa nchini ni mwendelezo wa michezo mingine mingi ya bahati nasibu itakayokuja baadaye.

“Kampuni yetu inao uzoefu wa muda mrefu kuendesha michezo ya Bahati Nasibu na tutahahakikisha watanzania  wananufaika na mchezo huu pia tutachangia pato la taifa kwa njia ya kodi kupitia mchezo huu.Aliongeza kuwa  uchezeshaji wa mchezo utakuwa wa wazi kupitia vyombo vya habari na mshindi atakuwa anatangazwa na kupatiwa fedha zake mara moja bila kuwepo urasimu wa aina yoyote.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubatisha ya Taifa,Abbas Tarimba aliwataka watanzania kuchangamkia fursa hii kwa kununua tiketi za kushiriki katika mchezo kutoka kwa mawakala waliosambaa nchini kote ili waweze kujishindia zawadi ya mamilioni ya fedha na kubadilisha maisha yao.

Tarimba aliwataka wananchi wasiwe na hofu ya kushiriki kwenye mchezo kwa kuwa unafanyika kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa na serikali “Wananchi wasiwe na wasiwasi kushiriki kwenye mchezo huu kwa kuwa fedha zao na kanuni za uendeshaji wa mchezo vinasimamiwa na serikali.

Alisema ujio wa mchezo huu nchini mbali na kuwanufaisha  washindi binafsi utachangia kupanue wigo wa ajira kwa Watanzania wengi watakaosimamia zoezi la ukatishaji tiketi katika vituo zaidi 20,000 vitakavyofunguliwa Nchi nzima.



Tiketi za mchezo huu zimeanza kuuzwa nchi nzima na wakati wa uzinduzi wa huduma za kampuni mkoani Dodoma wananchi wengi walijitokeza kununua tiketi za kushiriki na walishauri mtandao wa kuuza tiketi ufanyike kupitia hata kwenye simu za mkononi ili kuwawezesha wananchi wengi kushiriki kununua tiketi ambayo kila moja inauzwa shilingi 500/-.
Posted by MROKI On Friday, May 27, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo