Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akipeana mkono na Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa mara baada ya benki hiyo kuzinduwa hati fungani zinazoanza kuuzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (katikati) akizungumza na wanahabari hawapo pichani katika hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Kushoto ni Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha wa NMB, Waziri Barnabas na Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa (kulia).
BENKI ya NMB PLC imeanza kutoa hati fungani ya
NMB yenye riba ya 13% kwa yeyote mwenye nia ya kuwekeza na kupata faida nzuri.
Hii ni mara ya kwanza kwa NMB kutoa hati fungani ya namna hii
na inaweza kununuliwa kupitia matawi yote ya NMB au kwa mawakala wanaotambulika
kwa kiasi cha chini cha shilingi 500,000 (laki tano tu).
Kufunguliwa kwa hati fungani ya NMB kwa wananchi
ni matokeo ya kupata kibali kutoka mamlaka ya masoko ya mitaji nchini - Capital
Markets & Securities Authority (CMSA).
Wawekezaki wa hati fungani ya NMB watapata riba
ya asilimia 13 kwa mwaka itakayolipwa kila baada ya miezi sita kwa miaka mitatu
mpaka mwezi Juni 2019; Riba itakayotolewa itakatwa kodi ya mapato. Hati fungani
ya NMB inauzika pia, na mteja anaweza kuiuza kwa mnunuaji mwingine na kupata
fedha yake kabla ya kmukomaa kwa hati fungani – yaani miaka mitatu.
Wawekezaji wanaweza kuiuza hati fungani hiyo
kabla ya kukomaa katika soko la wazi kupitia mawakala wa soko la mitaji – kwa
kufuata misingi ya soko la hisa la Dar es Salaam.
Mkurugenzi mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker
alisema “Misingi ya NMB ni uwekaji fedha wa wateja wadogo lakini kuna njia
nyingi za kutunisha mfuko wetu, kwa hati fungani ya NMB, tunategemea kutunisha
mfuko kwa shilingi bilioni 20 huku tukiwa na ruhusa ya kuongeza mpaka kufikia
shilingi Bilioni 25. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Wawekezaji wengi wameonesha nia ya kuwekeza
kwenye hati fungani za hali ya juu, nasi tunachukua hii kama fursa muhimu na
hivyo kukidhi kiu yao kitu ambacho kitachangamsha pia uendelezwaji wa masoko ya
mitaji nchini na njia mbali mbali za kukuza mitaji.
Fulsa hii inaturuhusu sisi kutafuta fedha zaidi
ambazo zitasaidia kutoa mikopo mingi na nafuu kwa wateja.
Meneja Miradi na Ukuaji wa Biashara Soko la Hisa
la Dar es Salaam, Patrick Masusa, alisema “tunafuraha kuwakaribisha NMB katika
vitabu vyetu vya hati fungani.
Hii inachangamsha sana soko kuona taasisi kubwa
kama hii kuendelea kujitanua kwenye uwekezaji wa hati fungani. Hati fungani ya
NMB ni maalumu sana kwasababu ipo wazi kwa kila mtu na inaweza kununuliwa kupitia
matawi yote ya NMB nchini.
Na kwa uwekezaji kama huu, tunategemea kukuza
huduma hii zaidi kwa miezi na miaka ijayo.”
Hati fungani ya NMB itaanza kuuzwa kuanzia
tarehe 10 Mei, 2016 mpaka June 8 2016 na riba itaanza kulimbikizwa kuanzia
tarehe hii. Kununua hati fungani ya NMB, mteja anatakiwa kutembelea tawi lolote
la NMB kati ya matawi 175 nchini kote au kwa mawakala wanaotambuliwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kushoto) akizungumza na wanahabari katika hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB.
Baadhi ya maofisa na wafanyakazi wa Benki ya NMB pamoja na wanahabari wakifuatilia hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB.[/caption] Alisema wawekezaji hao wataanza kupata gawio lao la asilimia 13 kwa kiasi ulichowekeza baada ya miezi sita na litaendelea kutolewa kila baada ya miezi sita kwa kipindi cha miaka mitatu. Aliongeza kuwa baada ya kutimia miaka mitatu mwekezaji atalipwa fedha yake pamoja na asilimia 13 ya kiasi alichowekeza. Hati fungani hizo zitaanza kuuzwa kwa wananchi kuanzia Mai 10 hadi Juni 8, 2016 ambapo ofa itafungwa na utaratibu wa kupangwa kwa hati hizo kuanza. Wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuwekeza fedha zao hasa wale wanaohifadhi fedha bila kuzizalisha kwani wataziongezea thamani.
Mmiliki wa Blogu ya Father Kidevu, Mroki Mroki (kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kushoto) mara baada ya hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Baadhi ya maofisa na wafanyakazi wa Benki ya NMB pamoja na wanahabari wakifuatilia hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB.

0 comments:
Post a Comment