NA BASHIR NKOROMO
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM)
kimesema, hakuna mgogoro uiopo wa kukabidhiana kijiti cha Uenyekiti ndani ya
chama hicho na kuonya vyombo vya habari kuacha kupotosha umma.
"Napenda kuwahakikishia
na kusisitiza kuwa hakuna mgogoro wa kukabidhiana kijiti cha Ueneyekiti katika
CCM na wala hautakuwepo", amesema, Msemaji Mkuu wa CCM, Christopher Ole
Sendeka, katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari leo.
Katika taarifa hiyo, Sendeka
amesema, baadhi ya vyomo vya habari vimekuwa vikitoa taarifa potofu kuhusu
mchakato wa Mwenyekoti wa sasa wa CCM Dk. Jakaya Kikwete kukabidhi kiiti cha uongozi wa CCM kwa Rais Dk. John Magufuli
kama ilivyo mila na desturi ya CCM.
"Yamekuwepo madai eti
Mwenyekiti amekataa au anachelewesha kukabidhi kijiti. Hbari hiyo sio kweli
kabisa na ni kinyume chake, kwani Dk. Kikwete amekuwa akisisitiza kukabidhi
madaraka mapema iwezekanavyo. kwa ajili hiyo kwenye kikao cha Mei 3, 2016 alikataa
isiongezwe agenda nyingine ambazo zitalazimisha Mkutano Mkuu Maalum kuchelewa
kufanyika kwa sababu kwa sababu ya kukailisha maandalizi ya ajenda hizo",
alisisitiza Sendeka.
Sendeka alisema, dhamira ya
CCM kupanga kufanya Mkutano Mkuu Maalum Mwezi Juni 2016, ipo pale pale isipokuwa kilichoelezwa kwenye
kikao ni kukamilisha utaratibu wa kupata fedha za kugharamia mkutano huo na
kwamba mpango wa kutafuta fedha ukikamilika
tarehe ya mkutano huo Mkuu Maalum itatangazwa.
Alisema, CCM inawataka
wanachama wake wasihamanike wala
kubabaishwa na taarifa za upotoshaji
zinazofanywa na watu aliosema kuwa ni wenye nia mbaya na CCM. "Hawa ni wale wale ambao wamekuwa wakiiombea mabaya CCM bila
mafanikio", alisema Sendeka.
"Pia tunapenda kukanusha
madai ati kuwa Mwenyekiti Kikwete aliwatahadharisha wajumbe wa Kamati Kuu
kuhusu ukimya wa Ndugu Edward Lowassa. Hakuna wakati wowote kauli kama hiyo
aliitoa. Ni uzushi mtupu. Jina la Ndugu Lowassa halikutajwa kabisa na hakukuwa
na sababu za kulitaja", alisema Sendeka na kuongeza;
"Aidha tunakanusha madai
ya kufanyika mkutano baina ya Mwnyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli, Katibu
Mkuu wa CCM kuhusu uchaguzi wa Katibu wa
Kamati ya Wabunge wa CCM. Hapajawahi ufanyika mkutano wa aina hiyo siku yoyote
na mahali popote. hivyo madai ya kuwepo kwa tofauti baina ya viongozi wakuu
kuhusu nani achaguliwe kuwa Katibu wa wabunge wa CCM hayana msingi
wowote".
Sendeka alisema, Kamati Kuu
iliteua wabunge wanne kugombea na kuwaacha wabunge wa CCM kuamua na kwamba
kuhusisha viongozi na hasa kuzua kuwepo kutkuelewana ni jambo la kusikitisha na
kwamba ni taarifa yenye uongo, yenye nia ovu kwa CCM na viongozi wake.
"Tunapenda
kuwatahadharisha waandishi wa habari kuandika habari za ukeli waache kuzua
mambo yenye kupandikiza chuki na mgawanyiko usiostahili kuwepo ndani ya CCM na
kuyaeneza katika jamii, badala yake waheshimu maadili ya kazi yao",
alisema Sendeka.
0 comments:
Post a Comment