Nafasi Ya Matangazo

May 04, 2016

Meneja Rasilimali watu wa Airtel , Gabriella Kaisi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na  James Kwayu na Abubakar Nassor ambao ni wanafunzi wa vyuo waliofaidika na ajira kupitia ushirikiano kati ya Airtel na AIESEC Tanzania (chama cha wanafunzi vyuoni)  wenye lengo la kuwawezesha vijana waliokoa vyuoni kupata ajira katika makampuni mbalimbali kila mwaka.
***************
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imedhamini kongamano la ajira  kwa vijana wa chuo kikuu linaloandaliwa na AIESEC Tanzania  lenye lengo la kuwaweka pamoja waajiri (makapuni) na waajiriwa watarajiwa (wanafunzi)  kwa lengo la kuwapatia Fursa zitakazowasaidia katika kuendesha shughuli za kiuchumi.

Kila Mwaka AIESEC huandaa kongamano la ajira kwa vijana linaloshirikisha wanafunzi zaidi ya 1500 kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali nchini. Kuanzia mwaka jana Airtel  imejikita na kushiriki  katika kongamano hilo ikiwa ni sehemu ya kuendeleza dhamira yake ya kuwawezesha vijana wanaohitimu vyuoni kupata ajira.

Akiongea kuhusu mpango huo, Meneja Rasilimali watu wa Airtel , Gabriella Kaisi alisema”Tunayofuraha kuwa sehemu ya mpango huu kwa kushirikiana AIESEC Tanzania lengo likiwa ni kuwafikia na kuwaajiri vijana wenye vipaji kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali nchini. Tunaamini kila kijana ana nafasi ya kufikia ndoto zake  na ndio mana tunatoa fursa  kwa vijana kufanya kazi pamoja nasi. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

Mwaka jana tuliwawezesha vijana watatu wahitimu kutoka vyuo vikuu vya IFM pamoja na chuo kikuu cha Dar es salaam kupata ajira katika ofisi zetu za Airtel. Vijana hao ni pamoja na Abubakar Nassor ambaye anafanya kazi katika kitengo cha masoko James Kwayu yuko katika kitengo cha Huduma kwa wateja na Gerald Msafiri anafanya kazi katika kitengo cha mauzo.

Vijana hawa watapata nafasi ya kwenda kufanya kazi nje ya nchi katika makao makuu ya Airtel  nchini Kenya na India  kwa muda wa mienzi miwili kuanzia mwezi wa Mei hadi Julai 2016. Watakaporudi watapangia kufanya katika vitengo tofauti ili kupata uzoefu na mwanga zaidi aliongeza Kaisi

Akiongea kuhusu program hiyo, moja kati ya waliofaidika na mpango katika kitengo cha masoko, Abubakar Nassor alisema” najisikia furaha kuwa mwanachama wa AIESEC Tanzania kwani kumeniwezesha kupata fursa hii adimu ya ajira, uzoefu katika kazi na nafasi ya kujifunza katika kampuni kubwa ya simu duniani. Nimejipanga vyema kujifunza zaidi katika miezi 2 nitakayokuwa  nchini India na Nairobi,   nahaidi kuitumia fursa hii vyema ili kuweza kuzifikia ndoto zangu

Mwaka huu Airtel imejipanga kuendelea kuwafikia vijana wengi zaidi kwa kutoa ajira kwa vijana wengine watano ambao watafanya vizuri na kufaulu mitihani mbalimbali inayoendelea kwa sasa.  
Airtel itatangaza majina ya wanafunzi wengine watakaofudhu na kuchaguliwa kwa mwaka huu mara baada ya hatua za uajiri zitakapokamilika
Posted by MROKI On Wednesday, May 04, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo