Na
Joseph R Mkonyi.
Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam
(Dawasco), limeendelea na operesheni yake maalumu ya kukagua makazi pamoja na
viwanda kwenye maeneo mbalimbali ya jiji ilikutambua wezi wa Maji ndipo walipo
baini wizi mkubwa wa Maji kwenye eneo la kata ya Mchikichini mtaa wa Ilala kota
jijini Dar es salaam.
Akizungumza kwenye eneo la tukio Afisa biashara wa Dawasco Ilala Deogratius
Ngwandu amesema kuwa wamebaini wizi wa Maji nyumbani kwa bwana Amini Idd ambapo
alichepusha bomba la Maji lisipite kwenye Mita hivyo alikuwa akitumia huduma ya
Maji bure na pia alikuwa akiuza Maji kwa wakazi wenzake kwa bei ya shilingi 200
kwa ndoo bila kibali, hivyo wamemkamata na kumfikisha polisi kwa hatua za
kisheria.
“Tukiwa tunaendelea na operesheni yetu ya kubaini wizi
Maji kwenye maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam tumeweza kumkamata bwana
Amini Idd wa kata ya Mchikichini mtaa wa Ilala Kota akiwa amejiunganishia Maji
kwa kuchepusha bomba lisipite kwenye mita na kutumia Maji hayo bure na kuuza
kwa wakazi wenzake pamoja na matumizi yake binafsi hivyo kulikosesha Shirika
mapato lakini tunampeleka polisi kwa hatua za kisheria”, alisema Ngwa’ndu.
Kwa upande wa mtuhumiwa bwana Amini Idd amekiri
kuchepusha bomba la Maji lisipite kwenye mita nakuunganisha moja kwa moja
kwenye bomba pamoja naukuza Maji bila kibali kutoka Dawasco ila amedai kuwa alifanya
hivyo kutokana na hali ngumu ya maisha nakuomba Dawasco msamaha pamoja na
kuwasihi wananchi wengine wasiibe Maji kwa kujiunganishia kinyume cha
utaratibu.
“Ni kweli nilichepusha bomba la Maji lisipite kwenye
mita ilikukwepa gharama nakuuzia wakazi wenzangu bila kibali kutoka Dawasco kwasababu
ya hali ngumu ilikuwa najitafutia riziki ila naomba msamaha, kitendo
nilichokifanya nikinyume na sheria pia nawasihi watu wengine wanaotumia Maji ya
Dawasco kwa wizi waache kabla hawajakamatwa”, alisema Idd.
Dawasco inaendelea kuwasihi wakazi wote wa jiji la Dar
es salaam waliojiunganishia Maji kiholela kujisalimisha iliwaweza kutambulika
kwani operesheni ya kubaini wizi wa Maji ni endelevu kwa maeneo yote ya jiji la
Dar es salaam hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika .
Operesheni yakubaini wezi wa Maji kwenye maeneo yote
ya jiji la Dar es salaam ni agizo la waziri wa Maji na umwagiliaji Mh Geryson
Lwenge pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda kwa Dawasco .
0 comments:
Post a Comment