Nafasi Ya Matangazo

April 05, 2016

1Askofu E. A.Kalinga pamoja na mkewe Mch Christina A.Kalinga kwa pamoja wakishuhudia muujiza wa mtoto aliye zaliwa Baada ya maombezi, katika picha mtoto Baraka Peter Lugega akiwa amebebwa na Baba yake Bw. Peter Legega ,pamoja na Mama yake Eva Katikati Wakiwa Kanisani.Baada ya Bw. Peter Lugega kuponywa pepo la ulevi uliopindukia na mke wake aliyepoteza Mimba sita na alikuwa hajawahi kunyonyesha mtoto lakini baada ya kuombewa na kuponywa anashangaa sasa ananyonyesha mtoto aliyejifungua baada ya maombezi hayo.

Maeneo tulipo : Morogoro Road Kimara Temboni Wilaya ya Kinondoni kabla ya Mbezi mwisho, Saranga,hatua chache utaona kibao chetu barabara ni-Kushoto rangi ya blue bahari. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
6: Huduma zetu Kanisani:- Jumapili asubuhi saa 2:00 -4:30 watu wote kujifunza neno la Mungu ,Sunday School.

;saa 4:30-5:30 kusifu na kuabudu na mambo mengine (ibada ya kawaida) 5:30-6:30 maombi ya udhihilisho wa nguvu ya Mungu katikati ya kusanyiko (ibada) -kujazwa Roho Mtakatifu (watu wote) -kunena kwa lugha mpya(watu wote) -kuponywa magonjwa mbalimbali (watu wote) -kufunguliwa vifungo vya uovu vya asili,na laana mbalimbali za watu (watu wote) 2: Jumatano: Hii ni siku ya watumishi kuwepo Kanisani kuanzia Saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni kwaajili ya :- -Ushauri wa mtu mmojammoja (Canseling) -maombi ya kufungua vifungo vya uovu kwa watu mbalimbali na laana Mbalimbali -kuombea wagonjwa na kuponywa -kusikia shuhuda mbalimbali kwa watu Mungu alivyo watendea. 3: Ijumaa siku hii ya ibada inaanza saa 10:00- 12:00 jioni tunasifu na Kuabudu ,na kusikia neno la Mungu ,na Maombi.

Napenda kueleza kwa wale wenye mapenzi mema kwa huduma yetu .Sisi tumepata bure Tunatoa bure watu hawa tunao wahudumia ,au tulio wahudumia si matajiri ni watu wa kawaida kama umeguswa na huduma yetu unaweza kuchangia huduma hii ili iwafikie watu wengi zaidi.

Namba zetu za simu unaweza kutuma chochote,au kwa mazungumzo nasi Voda: 0767919056 - Tigo:0712964258 Airtel :0692567672.
2
Askofu E.A.Kalinga aliye simama upande wa kulia katika picha, wakiwa katika picha ya pamoja na Wachungaji. Baada ya kuwabariki katika Kanisa la Sinai Tanzania Mkoa wa Rukwa, Sherehe hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa Serikali pia ,aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga mjini Meja Mstaafu Bahati Matala ambaye wameshikana mikono kwa furaha pamoja na viongozi wa Kata ya Malangali Wilaya ya Sumbawanga Mjini wakiwa pamojana baadhi ya niongozi wa Kanisa.
3
Baadhi ya waumini ndani ya kanisa wakijifunza neno la Mungu kipindi cha Sunday School ambacho kimekuwa chenye baraka sana ya watu kulijua neno la Mungu kwa kina .
4
Askofu E.A Kalinga pamoja na mke wake Mchungaji Christina Kalinga waliokaa viti vya mbele pamoja na baadhi ya waumini wakiwa katika hafla ya pamoja wakisherehekea baada ya ubatizo katika Kanisa hilo. Hili ni jambo linalo leta furaha katika utumishi, baada ya kuwafundisha watu neno la Mungu na kuelewa na kukubali kubatizwa.Math 28:19-20;Mark 16:15-16.
5
Waumini waliobatizwa wakiwa katika picha ya pamoja na Askofu Kalinga na mke wake Mchungaji Christina Kalinga , wakisherehekea baada ya ubatizo wao uliofanyika kwa Mchungaji Sekela Mushi wa kanisa la Penuel lililoko Suka -Kimara Dar es Salaam.
6
Askofu E.A Kalinga akimbatiza Mmoja wa waumini waliokata shauri na kubatizwa na askofu huyo wa kanisa la Sinai Dar es salaam kwa ubatizo wa maji mengi (kuzamisha).
7
Askofu .E.A.Kalinga kulia akiwa katika picha ya pamoja na wanachuo wenzake wakati wa walipohitimu shahada ya Diploma, katika chuo cha Bibilia cha The Oasis Healing Bible College, kilichopo nyuma ya jengo la ubungo Plaza, karibu na stendi ya mabasi yaendayo mikoani hapa Dar es Salaam.
Posted by MROKI On Tuesday, April 05, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo