Mwakilishi
wa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo,Bw.David Kaijunga ambaye ni Afisa Misitu wa
Wilaya hiyo akikata utepe kuzindua kituo cha mauzo cha kampuni inayotoa umeme
wa jua ya Mobisol Tanzania mwishoni mwa wiki.
Mwakilishi
wa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo,Afisa Mazingira na Misitu wa wilaya ya
Bagamoyo,Bw.David Kaijunga(kulia) akipata maelezo baada ya kuzindua kituo cha
mauzo na usambazaji cha Mobisol kutoka kwa msimamizi wa tawi la Mobisol
Bagamoyo Gladness
Mlalatu.
Mwakilishi
wa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo David Kaijunga
(kushoto) akiongea mara baada ya Kuzindua ofisi ya Mobisol wengine pichani kutoka kulia ni Meneja
Maendeleo wa kampuni hiyo, Saad Lattf, Ofisa Mkuu Mwendeshaji Henrik Axelsson
na Meneja Mauzo
Tanzania Joseph
Zikheli.
Mwenyekiti
wa Bodi ya na
Mshauri wa Kampuni ya Mobisol akihutubia wageni waalikwa.
Ofisa
Mkuu Mwendeshaji wa Kampuni ya Mobisol, Henrik Axelsson (kushoto)
akimuonyesha Afisa
Maliasili na Mazingira wa wilaya ya Bagamoyo, David Kaijunga (Kulia) moja ya Televisheni inayotumia umeme wa jua unaosambazwa na kampuni hiyo,
wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofisi zake Wilayani Bagamoyo mwishoni mwa
wiki,wengine pichani ni maofisa wa kampuni hiyo.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Kampuni ya Mobisol wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa ofisi za
kampuni hiyo Wilayani Bagamoyo.
*************
Kampuni ya Mobisol Tanzania
inayozalisha nishati ya umeme wa jua kwa kutumia teknojia za kisasa
zilizobuniwa nchini Ujerumani mwishoni mwa wiki imefungua kituo cha kutoa
huduma zake mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
Uzinduzi wa kituo hicho ni
mwendeleo wa kampeni ya “Maisha ni Bora Zaidi na Mobisol” ambayo
imelenga kuwawezesha wananchi wengi wanaoishi maeneo ya vijijini ambako bado
kuna tatizo la nishati ya umeme kuunganishwa na umeme unaotumia nishati ya jua
unaopatikana kwa gharama nafuu na wa teknolojia ya kisasa ambapo kwa sasa
watawezeshwa kufanya malipo ya kupata huduma hii kwa awamu.
Akiongea juu ya kampeni
hii,Meneja Masoko wa Mobisol Tanzania, Allan Rwechungura amesema kuwa kampeni
imelenga kuboresha maisha ya wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini ambako bado
umeme wa gridi ya Taifa haujawafikia,ambako kwa sasa wataweza kufurahia maisha
kwa kutumia umeme unaotokana na nishati ya jua ambao wataupata kwa gharama
nafuu wanayoweza kuimudu.
“Kampeni hii ni moja ya mkakati
wetu wa kuunga mkono jitihada za serikali za kusambaza umeme wa gharama nafuu
maeneo ya vijijini na ndio maana tumepunguza gharama za kujiunganisha na
mtandao wetu ikiwemo kuweka mpango maalumu wa kulipia kwa awamu ili wananchi
wengi wanufaike na huduma hii muhimu na kuboresha maisha yao”.Alisema
Rwechungura.
Alifafanua kuwa mpango mpya wa
malipo ya kupata huduma za Mobisol mteja anatakiwa kulipia shilingi 999 kwa
siku ambapo akikamilisha malipo atapata umeme wa uhakika wenye nguvu
zinazoanzia 80W hadi kufikia 200W kulingana na mahitaji yake ambapo
ataweza kuutumia kwa vifaa vya nyumbani pia kampuni inatoa ofa ya kufuatilia
iwapo wateja wake wanapata huduma ya uhakika na iwapo kunakuwepo na matatizo
yanarekebishwa na wataalamu wake waliobobea katika ufundi wa mitambo
inayozalisha umeme wa jua.
Pia Rwechungura
alisema kuwa lengo kubwa la kutoa punguzo hili ni kuwawezesha watoto wanaoishi
maeneo ya vijijini kujisomea katika mazingira bora wakiwa na nishati ya umeme
pia unapunguza uharibifu wa mazingira ikiwemo pia kuwawezesha wakazi wa
vijijini kuboresha maisha yao kwa kufanya shughuli mbalimbal za uzalishaji
zinazohitajika kutumia nishati ya umeme.
Katika mkakati wa mwaka huu wa kusogeza huduma zake vijijini mikoa itakayofikiwa aliitaja kuwa mbali na Tabora ni Kagera,Dodoma, na mikoa mingineyo.Hadi mwishoni mwa mwaka jana zaidi ya familia 35,000 nchini Tanzania na Rwanda zilikuwa zimeunganishwa na nishati ya umeme wa gharama nafuu wa nishati ya jua wa Mobisol.
0 comments:
Post a Comment