NYOTA 18 wa kikosi cha Mbeya City Fc sambamba na
viongozi 7, alfajiri ya leo,
wamewasili salama jijini Tanga
tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Mgambo JKT uliopangwa kuchezwa jumapili
hii kwenye uwanja wa Mkwakwani.
Mara baada ya kuwasili na kuweka kambi kwenye hotel ya Sea
Breeze, kocha mkuu Kinnah Phiri, amezungumza na mbeyacityfc.com na kusema kuwa
anamshukuru Mungu kwa kuwawezesha kufika salama jijini hapa hasa baada ya safari ndefu yenye zaidi ya
kilomita 900.
Ilikuwa ni safari ndefu, ni
kilomita zaidi ya 900 kutoka Mbeya mpaka hapa, wote tuko salama tunamshukuru
Mungu kwa kutufikisha katika hali hii, jioni ya leo tutafanya mazoezi kwenye
uwanja wa Mkwakwani kwa jili ya kuweka sawa miili yetu pia kujaribu kuizoea kwa haraka hali ya hewa ya
Tanga, hapa kuna joto
hii ni tofauti kubwa na kule
tulipotoka alisema.
Kwa upande wake mkuu wa
kitengo cha utabibu Dk Joshua Kaseko,
amethibitisha kuwa hali za wachezaji hao ziko sawa na ataitumia nafasi ya mazoezi ya jioni ya leo kurejesha uimara wa misuli ya baadhi ya nyota ambao kwa namna moja ama nyingine
watakuwa wamepatwa na uchovu mkubwa.
Hakuna shaka wote wako sawa,
ila nitatumia mazoezi ya jioni ya leo
kama ambavyo programu ya mwalimu inasema ili
kuwaimarisha wale ambao miili yao itakuwa imepata uchovu mkubwa kutokana na safari, kuwasili mapema
imetusaidia kwa sababu katika hali ya kawaida mchezaji anapwasa apate japo saa
24 za kupumzika kabla ya kuingia kwenye mchezo alisema.
Baadhi ya nyota walisafiri kwa ajili ya mchezo huo ni pamoja na Juma
Kaseja,Hanningtony Kalyesubula,John Kabanda,Tumba Lui,Raphael Daud,Kenny Ally,Ditram
Nchimbi,Yohana Moriss,Meshack Samwel,John Jerome,Hamidu Mohamed na wengine .
0 comments:
Post a Comment