Mkulima
wa Shahiri katika kijiji cha Nangwa wilayani Babati Peter Nade akiwa amesimama
kando ya trekta lake analotumia kumrahisishia kazi zake za kilimo.
Wajumbe
wa Kamati ya Bunge ya Biashara,Viwanda na Mazingira wakiwa kwenye
mashamba ya wakulima wa Shahiri wilayani Monduli katika ziara waliyoifanya hivi
karibuni.
Wajumbe
wa Kamati ya Bunge ya Biashara,Viwanda na Mazingira wakiwa kwenye
mashamba ya wakulima wa Shahiri wilayani Monduli katika ziara waliyoifanya hivi
karibuni.
HAKUNA
ubishi kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa wananchi wengi wanaoishi barani Afrika
pia kilimo ni njia pekee ya kuwawezesha wananchi wengi kwenye jamii za Kiafrika
kujikwamua kiuchumi na kuwezesha nchi nyingi kupiga hatua kwa kuinuka kiuchumi
pia sekta hii inayo nafasi kubwa ya kupunguza tatizo la ajira ambalo
limekithiri hususani kwa vijana.
Pamoja
na fursa zilizopo kwenye sekta ya kilimo bado wakulima wengi barani Afrika ni
maskini wa kutupwa na wanakabiliwa na changamoto nyingi zinazowafanya waishi
maisha duni ya kushindwa kikidhi mahitaji yao na wengi wao mazao wanaozalisha
hayawatoshelezi pia kwa mahitaji yao ya chakula.Majanga ya kulia njaa kwenye
nchi nyingi za Kiafrika ni jambo la kawaida.
Wakati
tatizo la kukomboa maisha ya wakulima wadogo kimaisha kuendelea kuwa
kitendawili kisicho na jibu miaka miaka hadi miaka,nuru imeanza kuonekana
kutokana na kufunguliwa kwa milango ya uwekezaji wa aina mbalimbali ambapo kuna
baadhi ya makampuni yamewekeza barani Afrika ambayo tayari yameonyesha kuwa na
dhamira ya kufanya kazi na wakulima wadogowadogo wanaozalisha malighafi kwa
viwanda vinavyomilikiwa na makampuni hayo badala ya kukamata ardhi na kuingia
kwenye sekta ya kilimo yenyewe.
Moja
ya kampuni ambayo imewekeza barani Afrika na imeanza kufanya kazi na wakulima
wadogowadogo kwenye nchi mbalimbali na ikiwa na mpango wa kupanua wigo wa
kusaidia wakulima wadogo ili waweze kuwa na uzalishaji wenye tija na kuiuzia
mazao ni SABMiller ambayo imefanya uwekezaji katika viwanda vinavyotengeneza
vinywaji. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Katika Baadhi ya nchi ambapo imeanza kufanya kazi na wakulima wadogo ikiwemo Tanzania ambapo tayari imeanza kufanya kazi na wakulima wa zao la Shayiri katika mikoa ya Kaskazini ya Arusha na Kilimanjaro tayari wakulima wameanza kuonja matunda ya ushirikiano huu kwa kuwa wanawezeshwa kuendesha kilimo cha kisasa,kupatiwa pembejeo,mbegu na wataalamu wa kutoa ushauri na wanakuwa na soko la uhakika kwa ajili ya kuuza mazao yao.
Peter
Nade ,mmoja wa wakulima wa zao la Shayiri wilayani Babati Mkoani Arusha na baba
mwenye watoto sita anatoa ushuhuda wa maisha yake yalivyokuwa hapo awali kabla
hajaanza kilimo cha zao la Shayiri“katika miaka ya nyuma nilikuwa mkulima wa
zao la mahindi katika kipande kidogo cha ardhi na maisha yalikuwa magumu
kutokana na udogo wa kipato na kutopata chakula cha kutosheleza mahitaji ya
familia yangu.Tangu nianze kilimo cha zao la Shayiri nikiwa kwenye kikundi
kinachoshirikiana na kampuni ya TBL Group maisha yangu yamebadilika
na kuwa bora “.
Nade
anaendelea kuelezea kuwa hivi sasa anamiliki shamba la ekari 200 na anafanya
kilimo cha kisasa akiwa na nyenzo za kisasa za kilimo na anawezeshwa
kuendesha kilimo cha Shayiri kwa kujiamini kwa msaada anaopata kutoka kampuni
ya Tanzania Breweries Limited.
Jambo
la kufurahisha analolielezea Nade ni kuwa maisha yake yamebadilika
kuwa bora ambapo kwa sasa anamudu kuwasomesha watoto wake katika
shule nzuri wilayani Babati na anamiliki trekta linalomsaidia kurahisisha
kazi yake ya kilimo.
Mkulima
mwingine wa Shayiri wa Monduli Nainoto Maliaki ambaye ni mjane amesema anamudu
maisha na kusomesha watoto wake na ameweza kujenga nyumba ya kisasa.Kwa upande
wake Onesmo Kway naye mkulima wa shayiri na yuko kwenye kikundi
kinachoshirikiana na TBL anasema kilimo cha Shayiri kimebadilisha kabisa maisha
yake ambapo kimemuwezesha kujenga nyumba nzuri na anawasomesha watoto wake bila
matatizo.
Shuhuda
wa mafanikio na zinazotia matumaini haziko kwa wakulima wa Shayiri wa Tanzania
peke yake bali ni kutoka nchi mbalimbali barani Afrika ambako
kampuni ya SABMiller imefanya uwekezaji na kuazisha mpango unaojulikana kama Go
Farming wa kushirikiana na wakulima wadogowadogo kwa kuwawezesha na kununua
mazao yao ambayo ni malighafi ya kutengenezea vinywaji vinavyozalishwa kwenye
viwanda vyake.
Lengo
kubwa la mpango huu ni kuinua maisha ya wakulima wadogowadogo,kuongeza kasi ya
kukua uchumi na kujenga mfumo mzuri na endelevu wa kupata malighafi
kwa ajili ya viwanda vyake vilivyopo kwenye nchi mbalimbali barani Afrika
Mpango
wa Go Farming haulengi kunufaisha wakulima wa Shayiri pekee bali pia wa mazao
mengine kama mtama na mihogo na katika siku za usoni wakulima wa zao la mahindi
watawezeshwa pia na inategemewa hadi kufikia mwaka 2020 zaidi ya wakulima nusu
milioni watakuwa wamewezeshwa sehemu mbalimbali duniani ambako kampuni imewekeza.
Matarajio
ya mafanikio ya mpango huu katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2020 yanaonyesha
kukua kwa asilimia 44 katika nchi 10 ambako umeanza kutekelezwa na inakadiriwa
kuwepo ongezeko la uzalishaji wa mazao kutoka tani 300,000 kufikia zaidi ya
tani 600,000.
Mpango
huu wa kampuni kutegemea kupata malighafi kutoka hapa nchini
umeungwa mkono na serikali za nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania kwa kuwa
unalenga kuinua hali za maisha za wananchi hasa wakulima ambao wana hali
duni,hali hii imepelekea baadhi ya nchi kuipunguzia kodi ya zuio kampuni
inapofanya uzalishaji kwa malighafi zilizonunuliwa ndani ya nchi .
Hivi
karibuni Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ilipata fursa ya
kutembelea wakulima wa zao la Shayiri wanaoshirkiana na TBL Group na baadhi ya
wajumbe wa kamati hii walipongeza mpango huu wa kushirikiana na wakulima kuwa
utaweza kuinua sekta ya kilimo nchini kwa haraka na kuboresha maisha ya
wakulima.
Huu
ni mfano wa uwekezaji wenye faida kwa watanzania kwa kuwa unaeleta mabadiliko
kwenye jamii na kubadilisha maisha ya wananchi wengi kuwa bora.
0 comments:
Post a Comment