Wafanyakazi wa kiwanda cha TBL
cha Arusha wakifanya mazoezi ya kukimbia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Afya
Kwanza mwishoni mwa wiki
Kampeni ya TBL Group imezindua kampeni ya kuimarisha afya za
wafanyakazi wake wote ambapo wanashiriki kufanya mazoezi ya mwili sambamba na kupatiwa kupatiwa elimu inayohusiana na lishe
bora na matumizi ya vyakula visivyo na athari.
Afya Kwanza ambayo imeanzia kwa wafanyakazi waliopo Makao makuu na
viwanda vilivyopo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki imezinduliwa katika
kiwanda cha Arusha na kushirikisha wafanyakazi wa kiwanda hicho.
Msimamizi wa Programu hii ,Julieth Mgani alisema kuwa itakuwa endelevu
na wafanyakazi wameonekana kuifurahia katika kipindi cha muda mfupi tangia
ianzishwe
Wafanyakazi hao wa TBL Arusha wakifanya mazoezi ya viungo.
Wafanyakazi
wa TBL kiwanda cha Arusha wakimsikiliza mtaalamu wa lishe huku wakijipatia
matunda baada ya kufanya
mazoezi ya kuimarisha viungo vyao wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Afya Kwanza iliyofanyika
kwenye kiwanda hicho eneo la Themi jijini Arusha mwishoni mwa wiki
Meneja
Uendeshaji wa taasisi ya AAR Insurance Tanzania Ltd, Dk Harold Adamson
akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha TBL mkoa wa Arusha juu ya umuhimu wa
kuimarisha afya zao kwa kufanya mazoezi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Afya
Kwanza uliofanyika kiwandani hapo mwishoni mwa wiki
Wafanyakazi wa kiwanda cha TBL cha Arusha wakifanya mazoezi ya kukimbia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Afya Kwanza mwishoni mwa wiki
0 comments:
Post a Comment