WASANII wa muziki mbalimbali
hapa nchini, Jumamosi hii wanatarajiwa kukinukisha vilivyo katika Viwanja vya
Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam, katika tamasha la Amsha Mama
Festival.
Akizungumza kwa niaba ya
wasanii wenzake, Balozi wa tamasha hilo Khalid Ramadhani ‘Tundaman’,
ambaye amepewa Ubalozi huo kupitia waandaaji wa tamasha la (AFWAB)
AMSHA MAMA Festival 2016, lililo chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa lebo ya Candy
na Candy Records Joe Kariuki, alisema tamasha hilo linalotarajiwa
kufanyika Machi 5 mwaka huu katika uwanja wa Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
Tundaman na Muandaaji wa
tamasha hilo Kariuki, wamesema kwamba maandalizi ya shoo hiyo tayari
yameshakamilika kwa kiasi kikubwa hivyo angependa kutumia fursa hii kuwaalika
wakazi wote wa jiji la Dar, kujumuika siku hiyo kushuhudia burudani mbalimbali
zitakazotolewa na wasanii kibao ambao tayari wemedhibitisha kufanya makamuzi
siku hiyo.
“Tunapenda kuwaalika
Watanzania wote kwa ujumla siku ya jumamosi hii ya Machi 5, mwaka huu waje kwa
wingi katika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar Salaam, ili
tujumuike kwa pamoja katika tamasha la kuhamasisha wanawake kujikwamua katika
shughuli zao mbalimbali za kiuchumi.
Tamasha hili litakuwa ni la
wazi kwa maana kwamba watu wote watapata burudani kibao bila malipo yaani bure
kabisa hivyo waje kuwashuhudia wasanii kama, Khadija Kopa, Mr Blue, Snura,
Msaga Sumu, Ali Chocky na Tunda Man wakitoa burudani ya hali ya juu kwani
ulinzi na usalama siku hiyo ni wa uhakika,” alisema Tunda Man.
Kwa upande wake, Joe
Kariuki ambaye ni mratibu mkuu wa tamasha hilo ametumia muda huu kuongea na
baadhi ya akinamama wanaojishughulisha na biashara za vitu mbalimbali hususani
mama ntilie, wauza matunda na wauzaji wa mitumba ili nao wajitokeze kwa wingi
kuja kunadi bidhaa zao siku hiyo kwani hiyo ndiyo fursa yao ya kipekee ya
kujitangaza bure.
0 comments:
Post a Comment