Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Amina Juma Masenza kuwa mkuu wa mkoa wa
Iringa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Said Meck Sadiki kuwa mkuu wa mkoa
wa Kilimanjaro Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Amina Juma Masenza kuwa mkuu wa mkoa wa
Iringa Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Daudi Felix Ntibenda kuwa mkuu wa mkoa wa
Arusha Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Anne Kilango Malecela kuwa mkuu wa mkoa wa
Shinyanga Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Zelote Steven Zelote Kamishna Msaidizi
Mwandamizi Mstaafu wa Polisi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha
Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu kuwa mkuu wa mkoa wa Kagera
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na kutoa maagizo kwa wakuu wote wa mikoa
aliowaapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
Wakuu
wa mikoa wakila kiapo ambacho kitakua muongozo mkuu katika utendaji wao wakazi
Baadhi
ya Wakuu wa mikoa wakitia saini kiapo ambacho kitakua muongozo mkuu katika
utendaji wao wakazi
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika
picha ya pamoja na Wakuu wapya wa mikoa mbalimbali nchini aliowateua hivi karibuni. Wengine katika
picha ni viongozi mbalimbali wa ngazi za juu Serikalini.
******************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 15 Machi, 2016 amewaapisha wakuu wa mikoa 25, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA).
Walioapishwa na Mikoa yao katika mabano ni Said Meck Sadiki
(Kilimanjaro), Joel Nkaya Bendera (Manyara), Dkt. Rehema Jonathan Nchimbi
(Njombe), Said Thabit Mwambungu (Ruvuma), Mhandisi Evarist Welle Ndikilo
(Pwani), Magesa Stanslaus Mulongo (Mara), Amina Juma Masenza (Iringa), John
Vianney Kitayomba Mongella (Mwanza), Halima Omary Dendegu (Mtwara), Daudi Felix
Ntibenda (Arusha), Amos Gabriel Makalla (Mbeya), Jordan Mugirage Rugimbana
(Dodoma) na Aggrey Deaisile Joshua Mwanri (Tabora).
Wengine ni Godfrey Weston Zambi (Lindi), Kebwe Steven Kebwe (Morogoro),
Anne Kilango Malecela (Shinyanga), Anthony John Mtaka (Simiyu), Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Zelote Steven Zelote (Rukwa), Paul Christian
Makonda (Dar es salaam), Martine Reuben Shigela (Tanga), Meja Jenerali Mstaafu
Salum Mustafa Kijuu (Kagera), Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga
(Katavi), Meja Jenerali Emmanuel Edward Maganga (Kigoma), Mhandisi Mathew John
Mtigumwe (Singida).
Rais Magufuli pia amewaapisha Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa hapa nchini (TAKUKURU) Kamishna wa Polisi Valentino Longino
Mlowola na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Japani
Kidata.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mteule Luteni Mstaafu Chiku Galawa
hakuapishwa leo kutokana na dharula ya
kikazi, na tarehe ya kuapishwa kwake itapangwa siku nyingine.
Mara baada ya kukamilika kwa kiapo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa ujumbe kwa Wakuu wote wa Mikoa, ambapo
amewataka kwenda kufanya kazi kwa kujiamini na kujielekeza kutatua kero za
wananchi.
Maagizo mengine ya Rais Magufuli ni pamoja na kuwataka wakuu hao wa
mikoa kusimamia ulinzi na usalama katika mikoa yao, na Kuhakikisha watu
wanafanya kazi hususani vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa.
"Haiwezekani Vijana wawe wanashinda vijiweni wanacheza pool,
wakati wazee na akina mama wapo mashambani wanalima. Kawahimizeni wafanye kazi,
wasipofanya kwa hiari walazimisheni kufanya kazi" Alisema Rais Magufuli
Agizo jingine la Dkt. Magufuli ni kuwataka kusimamia udhibiti wa fedha
za umma katika halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji na ametoa siku
15 kwa halmashauri hizo pamoja na Wizara na Taasisi za Serikali kuondoa majina
ya wafanyakazi hewa katika orodha za mishahara ya watumishi wa umma.
Rais Magufuli pia ametaka Wakuu wa Mikoa wakasimamie utekelezaji wa
Elimu Bure ya kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne, ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha shule zina madawati na majengo ya kutosha.
Dkt. Magufuli amewasisitiza wakuu hao wa Mikoa kutosita kufanya maamuzi
na kuchukua hatua haraka, huku akitaka wawasimamie ipasavyo wakuu wa wilaya,
wakurugenzi wa halmashauri, Makatibu Tarafa na Watendaji wa kata na Vijiji ili
watekeleze wajibu wao na waache kuwaonea wananchi wa chini.
0 comments:
Post a Comment