GOLIKIPA wa zamani wa Simba Abel Dhaira (28) amefariki dunia.
Dhaira raia wa Uganda amefariki baada ya kuugua ugonjwa wa saratani akiwa nchini Iceland akiitumikia klabu ya IBV Vestmanaeyjar.
Dhaira alianza maisha yake ya soka katika klabu ya Walukuba ya jijini Jinja na kujiunga na Express, kisha akaenda URA kabla ya kuja kujiunga na Simba SC.
Aliitumikia klabu ya IBV Vestmanaeyjar football club inayoshiriki ligi ya Iceland premier league mpaka kifo chake.
0 comments:
Post a Comment