Waziri
wa Wizara ya Fedha na Mipango Philip Mpango akizungumza na waandishi wa
habari mda mfupi uliopita katika ukumbi wa mikutano wa wizara ya Fedha
jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Mapato na Matumizi ya Serikali kwa
Mwezi Machi mwaka huu, ambapo Mapato ya Kodi (TRA) shilingi
1,283,274,000,000. Mapato yasiyo ya kodi ni shilingi 77,504,000,000.
Mapato yatokanayo na vyanzo vya halmashauri ni shilingi 43,490,000,000
Jumla ikiwa ni 1,404,268,000,000. Pia amesema kuwa Serikali inatarajia
kupata mikopo na misaada ya mifuko ya Basket na Miradi ya maendeleo
kutoka kwa washirika wa maendeleo shilingi 71,200,000,000.
Waziri
wa Wizara ya Fedha na Mipango Philip Mpango akizungumza na waandishi wa
habari mda mfupi uliopita jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu
Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Ashantu Kijaji akiwa katika
mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
UFAFANUZI WA
MAPATO NA MATUMIZI
YA SERIKALI KWA MWEZI MACHI, 2016
A:
MAPATO
(i)Mapato
ya kodi (TRA) shilingi 1,283,274,000,000
(ii)Mapato
yasiyo ya kodi shilingi 77,504,000,000
(iii)Mapato
yatokanayo na vyanzo vya Halmashauri shilingi 43,490,000,000
Jumla shilingi
1,404,268,000,000
(iv)Tunatarajia
pia kupata mikopo na misaada ya mifuko ya Basket na miradi ya maendeleo kutoka
kwa washirika wa maendeleo shilingi 71,200,000,000
B: MATUMIZI
1. Mishahara
(a)Watumishi
wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa shilingi 484,057,177,680 ikijumuisha
malimbikizo ya shilingi 9,479,389,384 na hasa kwa walimu katika Halmashauri 154
(b)Watumishi
wa Taasisi na Wakala za Serikali shilingi 97,985,822,320 ikijumuisha
malimbikizo ya shilingi 518,822,320 kwa Taasisi na Wakala 24 na hasa sehemu
kubwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Jumla ya mishahara ni
shilingi 582,043,000,000
2.
Posho
ya chakula kwa ajili ya vyombo vya ulinzi na usalama shilingi 43,556,500,000.
3.
Ruzuku
ya Vyama vya Siasa shilingi 1,433,583,000
4.
Posho
ya Madaktari wanafunzi 1608 shilingi 1,721,000,000.
5.
Wizara
ya Afya Ununuzi wa madawa na vifaa tiba shilingi 2,597,961,000
6.
Mikopo
ya wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa semista ya tatu shilingi 57,040,000,000
7.
Kutekeleza
mpango wa Elimu bure shilingi 18,777,000,000
8.
Mapato
ya ndani kwa Halmashauri kwa ajili ya miradi na uendeshaji wa ofisi shilingi
43,490,000,000
9.
Madeni
ya watumishi wasio walimu katika Halmashauri shilingi 3,618,900,612
10.
Miradi
ya umeme shilingi 73,252,000,000
-
Wakala
wa Umeme Vijijini shilingi 24,020,000,000
-
Mradi
wa Umeme Kinyerezi I shilingi 43,800,000,000
-
Mradi
wa kufua umeme makambako – Songea shilingi 5,482,000,000
11.
Malimbikizo
ya madeni ya Makandarasi wa barabara shilingi 166,905,919,730
12.
Miradi
ya Maji shilingi 10,951,000,000
13.
Mfuko
wa Reli shilingi 2,651,000,000
14.
Fidia
kwa wananchi kupisha mradi wa Kurasini Trade and Logistic Hub shilingi
3,048,904,930
15.
Mradi
wa Ununuzi wa dawa na vifaa Tiba (ORIO) shilingi 2,106,657,644
16.
Mfuko
wa kuchochea maendeleo ya jimbo shilingi 5,124,997,500
0 comments:
Post a Comment