Meya Mpya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita Charles
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeiangusha Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa Meya wa jiji la Dar es Salaam hii leo.
Katika uchaguzi uliofanyika leo katika Ukumbi wa Karimjee, huku pakiwa na ulinzi mkali ndani na nje ya ukumbi huo, madiwani walimchagua Diwani wa Kata ya Vijibweni Manispaa ya Temeke, Isaya Charles kwa kura 84 dhidi ya kura 67 za mgombea wa CCM Yenga Omary.
Kaimu
Mkurugenzi Jiji la Dar es Salaam, Sara Yohana alitangaza matokeo ya kura hizo na kusema kuwa kura zilizopigwa zilikuwa 158 kura zilizoharibika zilikuwa 7 na kura halali zilikuwa 151.
Katika uchaguzi huo wajumbe wa tano ambao walikuwa ni kutoka CCM hawakuweza kuhudhuria na kupiga kura.
Meya wa Jiji Isaya Charles aliwashukuru
wapiga kura wake wa kata ya Vijibweni kwa kumchagua kuwa Diwani pamoja
uongozi wa chama chake kukubali kumpa nafasi ya kugombea kiti hicho.
“Nimejipanga
kuleta maendeleo katika sekta ya elimu pamoja na kupambana na kero ya
foleni katika jiji letu na nitahakikisha wananchi wote maskini
wanafaidika na mapato ya jiji hili ikiwemo kuendeleza miundombinu
mbalimbali ,”alisema Charles.
0 comments:
Post a Comment