Nafasi Ya Matangazo

March 10, 2016

Mratibu wa Kitaifa wa Uzazi Salama, Dr Koheleth Winani ( kulia) na Mkurugenzi Msaidizi Mkazi wa Center for Disease Control (CDC) Tanzania, Dr Maestro Evans wakipongezana baada ya kuzindua namba maalumu itakayowawezesha watoa huduma za afya kuwasajili kina mama wajawazito na wenye watoto kwenye huduma itakayowapa taarifa mbalimbali za afya bure ijulikanayo kama  “Wazazi Nipende”.  mradi wenye lengo la kupunguza idadi ya vifo vya kina mama wajawazito na watoto. Akishuhudia ni Meneja Huduma za Jamii Airtel, Hawa Bayumi
Mratibu wa Kitaifa wa Uzazi Salama, Dr Koheleth Winani (wa kwanza kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati uzinduzi wa namba maalumu itakayowawezesha watoa huduma za afya kuwasajili kina mama wajawazito na wenye watoto kwenye huduma itakayowapatia taarifa mbalimbali za afya bure ijulikanayo kama “Wazazi Nipende” inayotolewa na Airtel pamoja na mHealth Tanzania chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya.  Katikati ni Meneja Huduma za Jamii Airtel, Hawa Bayumi akifatiwa Mkurugenzi Msaidi Mkazi wa Center for Disease Control (CDC) Tanzania, Dr Maestro Evans
***************
Airtel Tanzania kwa kushirikiana na mHealth Tanzania washerehekea kuanza kwa mwaka wanne wa ushirikiano wao wa kutoa taarifa za afya kwa wa mama wajawazito na watoto kwa njia ya  ujumbe mfupi kupitia program ijulikanayo kama “Wazazi Nipendeni”  kwa  kuzindua namba maalumu (USSD) itakayowawezesha watoa  huduma za afya  kuongezea ufanisi katika kutoa na huduma kwa mama na watoto

Airtel Tanzania imekuwa kampuni ya kwanza kushirikiana na mHealth Tanzania katika kuwawezesha wateja wake nchi nzima kupata tarifa za afya bila gharama zozote.

Katika mwendelezo wa kuboresha huduma hii, Airtel inayofuraha kutangaza teknokalogia mpya  itayowawezesha watoa  huduma za afya kuandikisha kina mama wajawazito na watoto  kwenye huduma ya “Wazazi Nipendeni” kupitia  namba maalumu (USSD code) kwa haraka na urahisi zaidi.

Namba hiyo maalumu itawawezesha maelfu ya watoa huduma za afya katika vituo mbalimbali kuwasadia wamama wajawazito, wa mama wenye watoto wadogo, watoto wadogo pamoja na wasaidizi wao kujiandikisha na huduma ya bure ya ujumbe mfupi wa taarifa za afya na kuwakumbusha tarehe za kuhudhuria kliniki

Akiongea kwa niaba ya Airtel,  Meneja Huduma za Jamii, Hawa Bayumi alisema “Tunajivunia kuwa sehemu ya mpango huu kwani tunaamini upatikanaji wa taarifa za afya ni muhimu  hivyo tunawawezesha kinamama  wajawazito na wenye watoto wadogo kupata taarifa hizi kupitia simu zao za mkononi wakiwa majumbani kwao bila gharama zozote.  katika kuhakikisha idadi kubwa ya  kila mama wanajiandikisha kwenye huduma ya Wazazi Nipendeni  leo tunazindua rasmi namba maalumu kwa watoa huduma za afya kufanya usajili,  lengo letu nikuhakikisha tunajenga utamaduni wa watu kufatilia afya zao.

huduma hii ya “ Wazazi Nipendeni” itawawezesha watakao jiunga kupata ujumbe mfupi wenye taarifa za afya 4  kwa wiki,  tunaamini kwa kufanya hivyo tutawawezesha wamama wajawazito na watoto kuzingatia afya bora wakati wote. aliongeza Singano

Naye Mtoa huduma za afya  wa kituo cha afya Vingunguti, Mosi Mohamed alisema” sasa anaweza kutumia namba hiyo maalumu  kusaidia jamii inayomzunduka kujiunga na huduma ya ujumbe mfupi wa bure ya Wazazi Nipendeni kwa urahisi akiwa mahali popote.

Akiongea kwa niaba ya Wizara ya Afya, Mratibu wa Kitaifa wa Uzazi Salama, Dr Koheleth Winani alisisitiza umuhimu wa kutumia teknologia ya mawasiliano  katika kupunguza vifo vya wamama  wajawazito “ utoaji wa taarifa muhimu za afya na kutoa ushauri kwa kina mama wajawazito na wenye watoto wadogo kunasaidia kujenga jamii yenye afya bora.  Huduma hii mpya ya namba maalumu itaboresha na kuongeza ufanisi mkubwa kwa watoa huduma wa afya nchi” alisema.

Huduma ya Wazazi Nipendeni inashirikisha washirika wengine zaidi ya 30 katika maeno mbalimbali  wakiongozwa na Wizara ya Afya, 


Ripoti inaonyesha  tangu kuanzishwa kwa huduma hii zaidi ya watu million 1.25 wamejiunga na huduma hii ya Wazazi Nipendeni kutoka katika mitandao mbalimbali. Kati yao zaidi ya 250,000 ni watumiaji wa Mtandao wa Airtel wamepokea ujumbe mfupi wa bure zaidi ya million 18 wenye ushari wa kiafya.
Posted by MROKI On Thursday, March 10, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo