Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Kikuu cha St Joseph Dar es Salaam leo na kuwataka kurejea darasani huku malalamiko yao yakitafutiwa ufumbuzi.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St Joseph, Dar es Salaam wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako leo.
***************
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi,
Profesa Joyce Ndalichako ameingilia kati mgogoro wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
St. Joseph Dar es Salaam, waliogomea kufanya mitihani na kuwataka warejee
madarasani wakati matatizo yao yakishughulikiwa.
Wanafunzi hao walikuwa katika siku ya tatu ya
mgomo wao jana ambapo pamoja na mambo mengine walikuwa wakilalamikia mapungufu
yaliyopo chuoni hapo ikiwa ni pamoja na maabara za kufanyia mafunzo kwa
vitendo, matatizo ya kiutawala, mitaala ya kufundishia pamoja na ada.
Waziri Prof. Ndalichako aliyewasili Chuoni hapo
majira ya Saa 3 asubuhi na kuanza kufanya ziara kukagua mazingira ya
kufundishia ya chuo hicho kwa kutembelea maabara zote chuoni hapo na kasha
kwenda kuzungumza na utawala, Serikali ya wanafunzi na mwisho alihutubia
wanafunzi wote.
Aidha ameiagiza Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU),
chini ya Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Yunus Mgaya kufuatilia na kuchunguza
kwa makini madai ya wanafunzi hao juu ya kuwepo kwa wahadhiri wasio na sifa
zinazotakiwa.
Aidha aliutaka uongozi wa chuo hicho chini ya
Makamu Mkuu wa Chuo wake Dk Gopal Raju Bhakasaju kuhakikisha yote ambayo
wameahidi kuyafanya wanayatekeleza mapema bila kuathiri masomo na hasa kama
yatafanyika.
0 comments:
Post a Comment