Nafasi Ya Matangazo

February 09, 2016

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba akimwinua mfugaji wa jamii ya Kimaasai, Ketepoi Nuru aishie katika Kijiji cha Kambara, Wilaya ya Mvomero mkoani Morogo, ambaye mifugo yake wakiwemo mbuzi, kondoo na ndama zaidi ya 80 wameuwawa kwa kukatwa mapanga na kundi la watu wanaodaiwa kuwa ni walinzi wa jadi wa Mwano jana. Waziri huyo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa na Mbunge wa jimbo la Mvomero, Suleiman Sadiq Murad 
 Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba akiwa mwenye majonzi wakati mfugaji wa jamii ya Kimaasai, Ketepoi Nuru ambaye mifugo yake imeuwawa akiwa ameketi chini. Mama huyo ni mjane. 
 Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba akiwa  na mwananke mjane mfugaji wa jamii ya Kimaasai, Ketepoi Nuru wakielekea kuangalia mifugo yake iliyouwawa.
 Waziri Mwigulu Nchemba na viongozi wengine wa wilaya ya Mvomero na mkoa wa morogoro pamoja na wananchi wa kijiji cha Kambara wakiangalia mifugo hiyo.
Mwigulu Nchemba na Mkuu wa wilaya ya Mvomero wakiwa ni wenye huzuni.
Posted by MROKI On Tuesday, February 09, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo