Katibu
mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mngereza
(katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel , Beatrice
Singano Mallya,( kushoto) na mshindi
wa Airtel Trace Music Stars Afrika , Nalimi Mayunga kwa pamoja
wakionyesha bango kuashiria uzinduzi msimu wa pili wa shindano la muziki
la Airtel Trace Music Stars nchini Tanzania
Mshindi wa
Airtel Trace Music Stars Afrika , Nalimi Mayunga akiimba wakati wa
uzinduzi wa msimu wa pili wa shindano la muziki la Airtel Trace Music
Stars litakalowapa nafasi
watanzania kushiriki na kuonyesha vipaji vyao na hatimae kujishindia
zawadi nono ikiwemo kurekodi video na wimbo na mwanamuziki nguli wa
Marekani , Keri Hilson
**************
Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel Tanzania leo imezindua rasmi msimu wa pili wa shindano lake kubwa la muziki la Afrika la
Airtel Trace Music Stars ambapo wanamuziki chipukizi nchini watapata nafasi yakuonyesha vipaji vyao ulimwenguni.
Msimu wa pili wa
Airtel Trace Music Stars kwa mwaka huu utasimamiwa na nguli mwanamuziki, mwandishi wa nyimbo ambae pia ni muigizaji maarufu Keri Hilson kutoka marekan.
Shindano la
Airtel Trace Music Stars msimu wa pili kwa mwaka huu litashirikisha nchi 9 barani Afrika zikiwemo Jamuhuri ya demokrasia ya Congo,
Gabon, Ghana, Kenya, Madagascar, Malawi,
Nigeria, Tanzania na Zambi. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Mshindi kutoka katika nchi zinazoshiriki atapata nafasi ya kushiriki katika Mashindano ya Afrika ambayo yanatarajiwa kufanyika
Lagos, nchini Nigeria mnamo mwezi Juni 2016.
Zawadi
nono ya mshindi wa Afrika ni pamoja na mafunzo ya kuwa mwanamuziki
bora kutoka kwa mwanamuziki nguli Keri Hilson ambapo yatafanyika
Atlanta nchini Marekani, pamoja na kurekodi wimbo na mwanumuziki huyo.
Mshindi hataishia kurekodi wimbo na Keri Hilson bali atapata nafasi ya
kurekodi wimbo pamoja na walioimba wimbo wa “Knock You Down” na kusaini
mkataba na kituo maarufu cha burudani cha
Trace TV na kufanyiwa promosheni kwenye baadhi ya vipindi vyake.
Akiongea
wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel , Beatrice
Singano Mallya alisema” Tunayofuraha kuzindua msimu wa pili wa shindano
la muziki la Airtel Trace Music Stars hapa Tanzania. Tunapenda kutoa
wito kwa vijana wetu watanzania wenye vipaji kutoka katika maeneo
mbalimbali kujitokeza na kushiriki katika mashindano haya.
Tunaamini
hili ni jukwaa la pekee litakalotoa FURSA na kuwawezesha
vijana wengi kubadili maisha yao na kuzifikia ndoto zao katika tasnia
ya muziki. Zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa shindano hili hapa
Tanzania kwa mwaka huu ni kama ifuatavyo Milioni 50 kwa mshindi wa
kwanza, million 3 na milioni 2 kwa washindi wa pili
na watatu “.
Nae Meneja wa Huduma za Ziada wa Airtel Bi Prisca Tembo alifafanua jinsi ya kushiriki alisema “washiriki wanatakiwa kupiga namba
0901002233
kwa kutumia simu zao za mkononi na kurekodi nyimbo zao kwa gharama ya
shilingi 150 tu kwa dakika ili kupata nafasi ya kuwa mwanamuziki bora
Afrika.
Baada ya kurekodi wimbo mshiriki atapata utambulisho wenye namba
ambayo itawawezesha marafiki
, ndugu , jamaa na wapenzi wa muziki wake kuweza kumpigia kura na
kupata nafasi ya kushinda katika fainali za Tanzania na hatimae
kushiriki katika mashindano ya Afrika. Kura zitapigwa kupitia ujumbe
mfupi kwenda namba 15594 alieleza Prisca Tembo, Meneja huduma
za ziada wa Airtel.
Mwaka
Jana Airtel Trace Music Star ilifungua njia kwa mwanamuziki chipukizi
Mayunga Nalimi na kumwezesha kuonyesha kipaji chake. Mayunga alishinda
katika mashindano ya Afrika na kuzawadia na mwanamuziki nguli wa
Marekani Akon kuwa mshindi wa Afrika. Nalimi alipata zawadi nono ikiwemo
dili ya kurekodi nyimbo yake na studio ya Universal pamoja na kupata
mafunzo na kurekodi wimbo wake na Akon nchini Marekani
, zawadi zenye thamani ya $500,000.
“Tunafurahi kwamba Mayunga amefanikiwa kurekodi wimbo wake wa kwanza wa
“Nice Couple” ambao umekuwa ukiongoza kwa kuchezwa kwenye radio pamoja na TV nchini. Pamoja na mafunzo kutoka kwa Akon ujulikanayo kama
“Please Don’t Go Away” ambao tunauzindua leo tunapozindua msimu wa pili wa shindano la Airtel
Trace Music Stars Tanzania”. alisema Tembo
0 comments:
Post a Comment