Kaimu
mtendaji mkuu wa wakala wa ufundi na umeme TEMESA Eng. Prisca Mkama akitoa taarifa
ya utendaji wa kivuko cha Magogoni kwa Waziri wa ujenzi,uchukuzi na mawasiliano
profesa Makame mbarawa kushoto na mkurugenzi wa ufundi dkt. William Nshama
kulia akifuatilia.
Mkuu wa
kivuko cha magogoni Eng. Charles Irege akimwonesha Waziri waziri wa ujenzi,uchukuzi
na mawasiliano profesa Makame mbarawa namna ya kufuatilia mapato ya kivuko cha
magogoni kwa njia ya elekroniki.
Mkuu wa
kivuko cha Magogoni Eng. Charles Irege akimwonesha Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano profesa Makame
mbarawa namna ya kukagua tiketi za kielekroniki kabla ya abiria kuruhusiwa
kuingia kwenye kivuko.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na mawasiliano profesa makame mbarawa mwenye suti akizungumza na wasafiri wa kivuko cha
magogoni eneo la kigamboni kabla ya kuanza safari kulia kwake ni Kaimu mtendaji
mkuu wa TEMESA Eng. Prisca Mkama. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano profesa Makame mbarawa mwenye suti akishuka kwenye
kivuko cha mv. kigamboni mara baada ya kukagua shughuli za kivuko hicho.
Abiria wanaotumia
kivuko cha Mv. Kigamboni wakielekea kupanda kivuko hicho kutoka magogoni kwenda Kigamboni.
**************
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh.Prof. Makame Mbarawa amewataka Wakala wa Ufundi
na Umeme nchini (TEMESA), kufunga mfumo kamili wa elekroniki katika kivuko cha Magogoni
ili kudhibiti mapato yanayopotea kiholela.
Amesema
takriban asilimia 20 ya abiria wanaotumia kivuko cha Mv Magogoni na Mv
Kigamboni wanavuka bila kulipa nauli hali inayoathiri mapato stahiki ya kivuko
hicho.
“Nawapa
miezi mitatu muwe mmefunga mfumo kamili wa kupokea nauli wa elektroniki ambao
utadhibiti ukwepaji wa kulipa nauli ili kuongeza mapato na kufikia shilingi
milioni 25 kwa siku,” amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri
Mbarawa amesema nia ya wizara yake ni kukusanya mapato stahiki kutoka katika vivuko
vyote ili kuwezesha kununua kivuko vipya
na kukarabati vivuko vingine kadri
iwezekanavyo.
Aidha
ameagia ufanyike uboreshaji wa bwalo la kupumzikia abiria upande wa magogoni
ili liweze kuhudumia watu wengi na katika hali nzuri na kuagiza uboreshaji huo
kuanza mara moja.
Amezungumzia
umuhumi wa wafanyakazi wa vivuko vya Magogoni na kigamboni kuwa na lugha nzuri
kwa abiria wao na kuwasaidia wale wenye mahitaji maaalum ili kuboresha huduma
ya usafiri ya vivuko hivyo.
Ameitaka
TEMESA kuweka mfumo wa tiketi za msimu zitakazowezesha wafanyakazi kulipa kwa
awamu moja au mbili kwa mwaka na hivyo kunufaika na punguzo maalum na kuondoa
usumbufu wa kulipa nauli kila siku.
Naye
Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA Eng. Prisca Mkama amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa
mapato ya kivuko cha Magogoni yataimarika hivi karibuni kufuatia mikakati
madhubuti wanayoifanya katika kuboresha huduma zao hususani eneo la Kigamboni.
Tariban
abiria elfu 60 hutumia kivuko cha Mv. Magogoni na Mv. Kigamboni kuvuka kwa siku
katika harakati za shughuli za kijamii na kibiashara.
0 comments:
Post a Comment