Nafasi Ya Matangazo

January 11, 2016

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimfariji Mama Maria Nyerere, Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,  alipokwenda nyumbani kwake Msasani kumfariji kufuatia kifo cha mkwe wake Marehemu Leticia Nyerere huko Maryland, Marekani. 

Rais John Magufuli amemtembelea na kumpa pole mke wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere kufuatia kifo cha Mkwewe Leticia Nyerere kilichotokea jana huko Maryland Marekani alikopelekwa kwa ajili ya kupata matibabu mapema mwezi huu.

Pamoja na kutoa mkono wa pole kwa Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani Jijini      Dar es Salaam, Rais Magufuli pia amewapa pole wanafamilia wote na amewaomba kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na ndugu yao.

Msemaji wa familia ya Mwalimu Nyerere Bwana Joseph Butiku amemueleza Rais Magufuli kuwa familia inaendelea na taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Marekani na itatoa taarifa baadaye.
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimfariji  na Mama Maria Nyerere, Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na wanafamilia  alipokwenda nyumbani kwake Msasani kumfariji kufuatia kifo cha mkwe wake Marehemu Leticia Nyerere huko Maryland, Marekani. 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Mama Maria Nyerere, Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na wanafamilia  alipokwenda nyumbani kwake Msasani kumfariji kufuatia kifo cha mkwe wake Marehemu Leticia Nyerere huko Maryland, Marekani. 
Posted by MROKI On Monday, January 11, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo