Wafanyakazi wa kampuni ya TBL Group
wanaofanyika kazi katika kiwanda cha kutengeneza bia cha bia cha Arusha na
Moshi wamepata fursa ya kupatiwa elimu
ya jinsia kutoka kwa
Mkaguzi Msaidizi wa jeshi la Polisi wa Dawati la Jinsia wilaya ya Kinondoni,
Inspekta Prisca Komba.
Baadhi ya wafanyakazi hao kwa
nyakati tofauti wameeleza kuwa wameweza kujua mengi kuhusiana na suala la
jinsia kwa ujumla na kupata fursa za kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana
na jinsia.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi wa Dawati la Jinsia
wilaya ya Kinondoni, Inspekta Prisca Komba akitoa mada wakati wa mafunzo ya
jinsia kwa wafanyakazi wa kiwanda cha TBL yaliyofanyika mjini Moshi leo
.Mafunzo haya yanaendelea katika viwanda vyote vilivyopo chini ya TBL Group nchini.
Mfanyakazi wa Kiwanda cha Tanzania Breweries
Limited kilichopo mjini Moshi, Siraji Muya, akichangia mada wakati wa
mafunzo ya jinsia kwa wafanyakazi wa kiwanda cha TBL yaliyofanyika mjini Moshi
leo .Mafunzo haya yanaendelea katika viwanda vyote vilivyopo chini ya TBL Group
nchini.
Mfanyakazi wa Kiwanda cha TBL cha mjini Moshi Venance
Mwakosya akichangia mada wakati wa mafunzo ya jinsia kwa wafanyakazi wa
kiwanda cha TBL yaliyofanyika mjini Moshi leo .Mafunzo haya yanaendelea katika
viwanda vyote vilivyopo chini ya TBL Group nchini.
0 comments:
Post a Comment