Meneja Uhusiano wa Dawasco, Everlasting Lyaro
SHIRIKA
LA Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), limerejesha huduma ya maji
safi katika maeneo yote yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu chini ya jiji la Dar
es Salaam, pamoja na baadhi ya maeneo ya
mji wa Bagamoyo mkoani Pwani ambayo yalikatiwa maji kwa saa 48 kupisha
uunganishaji wa maji katika bomba jipya.
Dawasco
ilikata maji kutatokana na mtambo wa kusukuma maji wa Ruvu Chini kuzimwa kwa
siku mbili kuanzia Jumamosi, Januari 23 hadi 24 mwaka huu kupisha Mkandarasi
Kampuni ya Synohydro kuunganisha bomba jipya na lile la zamani katika taki la
maji lililopo Wazo-Tegeta Dar es Salaam.
Meneja
Uhusiano wa Dawasco, Everlasting Lyaro, aliliambia gazeti hili kuwa huduma ya
maji katika baadhi ya maeneo ndio yataanza kupata maji kwa sasa na hali itakuwa
sawa kwa maeneo yote yote yanayo
hudumiwa na mtambo wa kusukuma maji wa Ruvu Chini kuanzia leo. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Aliyataja
maeneo ambayo yameanza kupata maji kuwa ni pamoja na,Bagamoyo ,Tegeta, Kawe,
Mbeki Beach, Msasani, Bunju, Boko, Mikocheni na maeneo mengine ya jirani na
maeneo hayo yaliyotajwa.
Lyaro
alisema kuwa hadi kesho maeneo mengi yataanza kupata maji kwani kukosekana kwa maji kwa siku mbili kumesababisha
mabomba kujaa upepo hivyo kuchelewesha kuwafikia wateja wao walio wengi.
Alisema
kazi hiyo ya kuunganisha bomba ilifanyika baada ya kukamilika kwa upanuzi wa
mtambo wa Ruvu Chini, hivyo kuondoa
tatizo la upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo yanayohudumiwa na
mtambo wa Ruvu chini.
Lyaro
alisema kuwa mradi huo ukikamilika mwezi feburai mwaka huu kiwango cha
upatikanaji maji yataongezeka jijini Dar es salaam kutoka lita milioni 182,000
hadi lita milioni 270,000 .
“Tunaelekea
kwenye hatua za mwisho za kupokea Maji mengi kutoka mtambo wa Ruvu Chini baada
ya kazi ya upanuzi inayoelekea kukamilika mapema mwezi February mwaka huu, na
kiasi cha Maji kitaongezeka kutoka wastani wa Lita Milioni 182,000
zinazozalishwa sasa hadi Lita Milioni 270,000,”alisema Lyaro.
Lyaro
alisema dawasco inawashukuru wateja wake kwa uvumilivu na bado inaendelea
kuwasihi kuwa wavumilivu hadi huduma ya maji itakapo rejea katika hali yake ya
kawaida. wakati mtambo huo ulipozimwa na maeneo mengi kukosa maji.
Maeneo
ambayo yalikumbwa na kadhia hiyo ya kukatiwa maji kutokana na kuzimwa kwa
mtambo huo wa Ruvu chini ni pamoja na mji wa Bagamoyo, vijiji vya Zinga, Kerege
na Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi Beach na Kawe.
Maeneo
mengine ni Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Kijitonyama,
Kinondoni, Oysterbay, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya Rufaa Muhimbili,
Buguruni, Chang’ombe na Keko.
0 comments:
Post a Comment