Barabara zinazoingia katika Daraja la Kigamboni.
Mkurugezi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau akimkaribisha Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa alipofanya ziara ya kuangalia maendekleoa ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni.
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Karim Mattaka akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (kushoto), wakati alipofanya ziara kuangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo linalotarajiwa kuanza kutumiaka rasmi ifikapo Februari 2016. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau.
Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (kushoto), akizungumza wakati alipofanya ziara kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni ambalo linalotarajiwa kuanza kutumiaka rasmi ifikapo Februari 2016. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau.
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Karim Mattaka akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kulia) TAZAMA PICHA ZAIDI HAPA
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Hamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (katikati), wakati waziri huyo alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi NSSF, Aboubakari Rajabu.
Waziri
wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (katikati),
akifafanua jambo wakati alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya
ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk.
Ramadhani Dau na kulia ni Ofisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Uhusiano na
Masoko wa NSSF, Salim Kimaro.
Meneja
Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Karim Mattaka
(katikati) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na
Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (kushoto) alipofanya ziara ya kukagua
maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa
NSSF, Dk. Ramadhani Dau.
Mkurugenzi
Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau na Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la
Kigamboni, Mhandisi Karim Mattaka wakitoa ufafanua kwa Waziri wa Ujenzi,
Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (kushoto).
Meneja
Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Karim Mattaka
akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame
Mbarawa sehemu zilizosali ambazo zinazofanyiwa matengenezoya mwisho
mwisho.
Waziri
wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (wa pili
kushoto), akikagua ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam
jana, daraja hilo linalotarajiwa kuanza kutumiaka rasmi ifikapo Februari
mwakani. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi NSSF, Aboubakari
Rajabu, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau, Meneja Mradi wa
Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Karim Mattaka na kushoto ni
Mkurugenzi wa Miradi na Uwekezaji NSSF, Yacoub Kidula.
Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (katikati), akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi NSSF, Aboubakari Rajabu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Hamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau (kushoto) akiagana na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa mara baada ya kukagua ujenzi wa Daraja la Kigamboni linalojengwa kwa ubia kati ya NSSF na Serikali.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (kushoto), akiagana na Ofisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Uhusiano na Masoko wa NSSF, Salim Kimaro.
Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa
(kushoto), akiagana na Ofisa Uwekezaji Mwandamizi, Zaina Kambagha.
Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa
(kushoto), akiagana na Meneja wa Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Karim mattaka.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja.
Waziri akiangalia maeneo yanayofanyiwa matengenezo.
DAR ES SALAAM, Tanzania
MENEJA Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, kutoka
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi Karim Mattaka amesema
kuwa ujenzi wa daraja hilo unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 31, 2016.
Mattaka aliyasema hayo jijini Dar es Salaam katika ziara
ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa
alipotembele daraja hilo.
Alisema wanaamini kuwa watamaliza kazi hiyo kwa wakati na
anawataka watanzania watarajie kuwa wataanza kulitumia daraja hilo ifikapo
mwezi Februari mwaka huu.
“Tunatambua kuwa wananchi wanakiu ya kulitumia daraja hili
na sisi tunawambia kuwa wasiwe na wasiwasi karibia tunamaliza yamebaki
matengenezo madogomadogo ambayo tunaamini kuwa tutayamaliza kwa haraka,”
alisema Mattaka.
Aidha alisema kutokwapo kwa wafanyakazi wenye ujuzi pamoja
na kunyesha kwa mvua kubwa miezi iliyopita kumechangia wao kushindwa kumaliza
kazi hiyo katika muda uliopangwa.
“Unajua hatuna wafanyakazi wa kutosha lakini pindi
tunapohitaji sasa wale wenye ujuzi ili tuongeze nguvu wanakosekana jambo hili
limechangia sana kuturudisha nyuma lakini pia kuna mvua kubwa ilinyesha kipindi
cha nyuma imeharibu maeneo baadhi ambayo tulikuwa tumemaliza hivyo tumejikuta
tunarudia upya kazi,” alisema.
Hata hivyo Mhandisi Mattaka alisema daraja hilo litakuwa na
urefu wa mita 680 na njia zitakuwa sita yaani tatu kwaajili ya kwenda na
nyingine tatu kwaajli ya kurudi.
“Licha ya daraja kuwa na mita hizi lakini barabara za awali
ambazo zitakamilika zitakuwa ni kilomita 2 na nusu na zitakuwa na njia sita
hizohizo, sisi tuhamu kubwa kuona watanzania walitumia daraja hili ndo maana
tunafanyakazi usiku na mchana,” alisema.
Naye Waziri Mbarawa amemtaka Mhandisi huo kukamilisha kazi
hiyo kwa muda uliopangwa ili wananchi waweze kulitumia na kuondoka na athari ya
usafiri wanayoipata sasa.
Mbarawa ambaye alifika katika daraja hilo majira ya saa nne
asubuhi na kutembelea mradi mzima amewataka wafanyakazi wote kwa ujumla
kufanyakazi kwa bidii ili wakamilishe mradi huo kwa muda uliopangwa.
0 comments:
Post a Comment