Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa (kulia) akimkabidhi kombe la tuzo ya mwajiri bora kwa Mkurugenzi
wa Raslimali Watu wa TBL Group,David Magese (Kushoto) katika hafla
iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa
Mlimani City mwishoni mwa wiki ambapo TBL iliibuka kwa mshindi wa tuzo hiyo kwa
mwaka 2015,(katikati) ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck sadiki.
Mkurugenzi wa Raslimali Watu wa TBL Group,David
Magese akionyesha kombe la tuzo ya mwajiri
bora ambalo kampuni yake imeibuka kuwa mshindi mwaka huu katika hafla
iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa
Mlimani City mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TBL group wakiwa katika
picha ya pamoja muda mfupi baada ya
kampuni yao kuibuka mshindi wa jumla wa tuzo ya mwajiri bora inayotolewa na
Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa
Mlimani City mwishoni mwa wiki.
Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa ( wa nne kutoka kushoto)
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali,viongozi wa Chama cha Waajiri
Tanzania (ATE) na wafanyakazi wa kampuni ya TBL Group muda mfupi baada ya
kuitunukia kampuni hiyo tuzo ya mwajiri bora kwa mwaka huu katika hafla
iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa
Mlimani City mwishoni mwa wiki. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
***********
KAMPUNI ya Tanzania Breweries
Limited Group imeibuka mshindi wa tuzo bora kwa mwaka
2015.Tuzo za mwajiri bora wa mwaka hutolewa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE)
nchini kwa kampuni inayokidhi vigezo mbalimbali vya mazingira mazuri ya
kufanyia kazi nchini.
Mgeni wa heshima katika hafla
ya Chama Cha Waajiri nchini kutunuku tuzo hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano
wa Mlimani City alikuwa ni Waziri Mkuu Mheshimiwa
Kassim Majaliwa.TBL ambayo pia inashikilia
tuzo ya Mlipa Kodi bora nchini pia katika shindano hili lililoshirikisha
makampuni mengi nchini ilishinda tuzo zingine tofauti ambazo ni Uzingatiaji
Kanuni Bora za Uongozi,Uongozi
na Utawala,Uzingatiaji wa Kanuni za Raslimali Watu ,Ubora na Uzalishaji,Kujali na
kuthamini walemavu na tuzo ya Taasisi Bora inayoongoza kwa Ukubwa .
Mwaka jana kampuni ya TBL
ilishinda tuzo ya jumla katika kipengele cha Mahusiano mazuri na wafanyakazi ambayo
inadhihirisha kuwa kampuni imeweka mazingira bora ya kufanyia kazi na inawajali
wafanyakazi wake katika ngazi zote.Tuzo hiyo pia ilitambua kuwa TBL imejenga
mazingira bora na uongozi makini unaozingatia vigezo bora vya ajira na kujenga
mazingira mazuri ya kazi kwa waajiriwa wake.
Akiongea wakati wa hafla
hiyo,Mkurugenzi wa Raslimali Watu wa TBL Group David Magese alisema kuwa kampuni
hiyo inao wafanyakazi 2,100 nchini kote wakiwa wanafanya kazi za ufundi,Mauzo
na Usambazaji,na katika vitengo mbalimbali vya biashara na kati ya hao wapo wenye
ajira za kudumu na ajira za muda.
Magese pia alisema kuwa
kampuni katika kuwajali wafanyakazi wake inao utaratibu wa kuwapatia
MOTISHA ambazo zimekuwa
zikitolewa kwa kuzingatia kigezo cha
utendaji wao bora wa kazi kwenye maeneo yao wanayofanyia kazi na utaratibu huu
umekuwa ukiwajengea wafanyakazi kufanya kazi kwa ufanisi na kuleta tija kwa
kampuni kutokana na kuwajali na kuthamini mchango wao katika maendeleo ya
biashara za kampuni.
Aliendelea kueleza kuwa TBL
inao mpango maalumu wa kutoa elimu ya tahadhari kwa wafanyakazi wake dhidi ya magonjwa
mbalimbali ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza kwa ajili ya kulinda afya za afanyakazi
na chini ya mpango huu imejipangia
utaratibu wa kutoa elimu ya afya
kuendana na siku za matukio mbalimbali yanayohusiana na afya na usimamizi wake unafanyika
kwa umakuni mkubwa chini ya wasimamizi wenye ujuzi unaostahili.
Magese pia alisema kampuni
imekuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo mbalimbali kwa wafanyakazi wake ambayo
yanawawezesha kufanya zao kwa ufanisi na
bila kusimamiwa.”Bajeti ya asilimia 50% ya kitengo cha Rasilimali watu
imekuwa ikitumika kwa ajili ya kutoa mafunzo ya kuwapatia ujuzi afanyakazi kwa
kuwa kampuni inaamini kuwa wafanyakazi bora na wenye ujuzi ndio nguzo katika
uzalishaji na kukuza biashara zake”.Alisema.
0 comments:
Post a Comment