Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na Jeshi la Polisi Nchi zima kupambana na watu watakaovunja sheria ya usafirishaji wa watu kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
************
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
JESHI la Polisi Nchini limewatahadharisha madereva watakaozidisha
idadi ya abiria kuliko uwezo wa chombo cha usafari kwani ni kosa
kisheria na watakaozidisha abiria kwenye vyombo vyao vya usafiri
watachukuliwa hatua za kisheria.
Operesheni hiyo inaanza leo baada ya tamko la Jeshi la Polisi na
kuanza kutekeleza kwa wale wote wataobeba abiria wengi tofauti na uwezo
wa basi, watachukuliwa hatua madereva wa daladala,mabasi ya mikoani
pamoja na magari aina ya Noah.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msemaji
wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba amesema kuwa Jeshi la polisi linaanza
operesheni ambayo ni endelevu na kuwataka watu wafuate sharia ya
ubebaji wa abiria.
Advera amesema kuwa katika kipindi hiki cha siku kuu Jeshi la
polisi limejipanga katika kuwadhibiti waendesha bodaboda kwa
wataopandisha watu zaidi ya wawili (mishikaki) kukiona cha mtema kuni
kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani.
Aidha amewataka wananchi kutoa taarifa za kihalifu katika msimu wa
sikukuu na uimarishaji wa ulinzi wa watu na mali zao na maisha yaweze
kuendelea baada ya sikukuu.
0 comments:
Post a Comment