Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya DCB, Edmund Mkwawa (wapili kushoto)
akikmakibidhi msaada wa vitanda vya kuzalishia wajawazito kwa Mganga Mkuu wa
Manispaa ya Temeke, Cylvia Mamkwe (kulia) katika hafla iliyofanyika Hospitali
ya temeke Dar es Salaam jana na kushuhudiwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya
Temeke, Dk Aman Malima (katikati), Muunguzi katika Hospitali hiyo, Deodata
Msoma na Meneja Masoko wa Benki hiyo, Boyd Mwaisame. Benki ya DCB ilikabidhi
vitanda 21 ikiwa ni saba kwa kila Hospitali ya Amana, Temeke na Mwananyamala
vikiwa na thamani ya Sh 17.5.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya DCB, Edmund Mkwawa (wapili kushoto) akikmakibidhi msaada wa vitanda vya kuzalishia wajawazito kwa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Cylvia Mamkwe (kulia) katika hafla iliyofanyika Hospitali ya temeke Dar es Salaam jana na kushuhudiwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke, Dk Aman Malima na Muunguzi katika Hospitali hiyo, Deodata Msoma. Benki ya DCB ilikabidhi vitanda 21 ikiwa ni saba kwa kila Hospitali ya Amana, Temeke na Mwananyamala vikiwa na thamani ya Sh 17.5.
Moja ya vitanda hivyo vya kuzalishia akina mama wajawazito.
Viongozi hao wakiangalia vitu hivyo.
**************
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo,
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Edmund Mkwawa alisema benki yake
imechangia vitanda 21 vya kuzalishia akina mama wajawazito vyenye thamani ya sh
Milioni 17.5 kwa Hospitali za Amana, Temeke na Mwananyamala ikiwa ni vitanda
saba kwa kila Hospitali.
“Tumekuwa na desturi ya kurejesha katika jamii
sehemu ya faida tunayoipata kila mwaka, na hadi sasa tumesha tumia zaidi ya sh
milioni 125 kwa kusaidia jamii vitu mbalimbali, tunaamini nah ii leo kwa kiasi
fulani utasaidia kuboresha utoaji huduma katika hospitali zetu,” alisema
Mkwawa.
Mkwawa alisema vitanda hivyo vitapunguza matatizo ya akina
mama yatokanayo na ukosefu wa vitanda vya kujifungulia.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dk Sylvia
Mamkwe kwa upande wake aliishukuru Benki ya DCB kwa msaad huo wa vitanda 21 na kusema utasaidia kupunguza maambukizi wakati wa uzazi.
Dk Mamkwe alisema pia vitanda hivyo vitazidi kupunguza vifyo vya mama na mtoto ambavyo vimetoka 59 kwa mwaka hadi kufikia nane kwa mwaka huu.
“Kutokana na misaada hii kama huu ambao tumeupokea
hii leo wa vitanda vya kujifungulia akina mama wajawazito kutoka Benki ya DCB,
na kuwa na wataalam tumepunguza vifo vya akina mama wajawazito kutoka 59 kwa
mwaka hadi nane kwa mwaka huu,”alisema Dk Mamkwe.
Aidha alisema kuwa msaada huo walioupata kutoka
Benki ya DCB umewafikia wakati muafaka kwani tayari wameanza kutumia jingo lao
jipya hivyo vitanda hivyo vitasaidia jitihada za kupunguza maambukizi ya mama
na mtoto ambayo hutokea wakati wa kujifungua.
0 comments:
Post a Comment