Mpiganaji Deo Kakuru akiwa na dada Joyce ndani ya FastJet wakitoka Mbeya keuelekea Dar es salaam
Dada Joyce akiwa ameketi kwa utulivu kwenye siti yake ndani ya ndege
Mpiganaji Deo Kkuru akiwa na dada Joyce mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam
Msamaria mwema Mama Rozi akimhudumia dada Joyce akiwa kitandani kwake Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha mifupa cha MOI katika wodi ijulikanayo kama Wodi ya Magufuli ghorofa ya tatu.
Dada Joyce akiwa wodini Moi.
***********
***********
Ndugu Wasamaria wema,
Tunapenda kutumia fursa hii kuwapa updates kuhusu dada
Joyce Mwambepo, mkaazi wa Sinde jijini Mbeya mwenye umri wa miaka 27 ambaye anaishi
na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 pamoja na mwanaye mwenye umri wa miaka 4.
Kwa
bahati
mbaya mwezi April mwaka jana dada huyu alipata ajali ya kugongwa na gari
ambalo dereva wake hakusimama kumsaidia. Ila kwa msaada wa wasamaria
wema alipelekwa hospitali ya
rufaa ya mkoa wa Mbeya ambako inasemekana alikaa kwa miezi mitatu bila
kupata
matibabu kwa kukosa fedha. Katika
uchunguzi wa awali ilibainika kuwa Joyce amevunjika miguu yote miwili,
hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia baada
ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa Mbeya baada ya kukosa pesa za matibabu.
Baada
ya
mwanahabari Deo Kakuru wa Mbeya kumgundua na kufanya juhudi za kutoa
taarifa za
dada Joyce katika mitandao mbalimbali, wasamaria wengi wa ndani na nje
ya nchi wakaguswa na kuchangia. Mungu mkubwa, kiasi kilichopatikana
(kiasi cha 3.2m/-)
kimewezesha dada Joyce kupelekwa Dar es salaam toka Mbeya kwa ndege ya
Fast Jet Alhamisi
iliyopita na moja kwa moja kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili na
kupokelewa katika kitengo cha MOI na kupatiwa kitanda katika wodi mpya
ijulikanayo kama Wodi ya Magufuli, ghorofa ya tatu chumba namba mbili.
Cha
kufurahisha ni kwamba Joyce aliweza kukaa kwenye kiti cha kusukumwa na hata
kwenye ndege aliketi kama kawaida, zoezi ambalo hata yeye anasema limemsaidia
kwani kwa mara ya kwanza hivi sasa ganzi miguuni inapotea taratibu na ukimgusa
anahisi mguso tofauti na ilivyokuwa awali.
Daktari
bingwa ameshaonana naye na kumpa matumaini ya kupona, hasa sehemu ya chini ya
uti wa mgongo wake ambao inasemekana una matatizo yaliyopelekea kubana mishipa ya fahamu na kufanya miguu ipooze.
Zoezi linalosubiriwa kwa sasa ni kupatiwa vipimo vya MRI ili kubaini kiufasaha
tatizo lake na hatimaye kupatiwa matibabu. Zoezi hili linatarajiwa kufanyika
wakati wowote kuanzia sasa.
Mpiganaji
Deo Kakuru amesharejea Mbeya na kijiti cha kumwangalia dada Joyce amekabidhiwa
Ankal ambaye anaomba Wasamaria wema waendelee kumuombea na kumsaidia kwa hali
na mali dada huyu ambaye ni yatima.
Kwa
bahati njema
Ankal alikutana na kuongea na Msamaria mwingine aitwaye Mama Rozi
ambaye anamuuguza mama yake mzazi aliyelazwa wodi moja na dada Joyce.
Msamaria huyu
amekubali kumsaidia dada Joyce kwa chakula na pia kumsaidia usafi maana
hapo
kitandani hawezi kuondoka.
Mungu kweli ni
mkubwa. Dada Joyce anatabasamu na kuongea vizuri tu. Anatoa shukurani sana kwa
wote waliomsaidia na wanaoendelea kumsaidia. Anasema hana cha kuwalipa ila kusema
ASANTE SANA na anamwomba Mola Muumba awazidishie pale patapopungua. Ameomba
anayeweza kumtembelea atafurahi sana maana hana ndugu hapa Dar es salaam.Pia
anawashukuru sana madaktari waliomhudumia vyema katika Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Mbeya ambao amesema hatowasahau kwa msaada wao.
Ankal amejitolea kuendelea kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce.
Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba+255 754 271266 kwa jina la Ankal.
AU mratibu-mwenza Deo Kakuru Msimu
Pia unaweza kuwasiliana moja kwa moja na dada Joyce kwa namba
0 comments:
Post a Comment