Mkuu wa Kitengo cha Sheria Balaza la Taifa la usimamizi wa mazingira Tanzania (NEMC), Manchale Heche akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam juu ya zoezi la Bomoabomoa maeneo ya miundombinu na maeneo yote hatarishi nakuwataka wananchi waliojenga katika fukwe za bahari Kingo za mito na mikondo ya bahari kuhamisha mali zao mapema.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Manispaa za jiji la Dar es salaam zitafanya zoezi la kuondoa wavamizi maeneo yote ya Mabondeni, kingo za mito na za Bahari, maeneo ya wazi, maeneo ya miundombinu na maeneo yote hatarishi zaidi ya 150 katika jiji la Dar es salaam. Bomoa bomoa ya leo inaendelea katika Bonde la mto msimbazi. Source:Michuzi Media
Wananchi wakitoa samani pamoja na vitu mbalimbali ndani ya nyumba zao ili kupisha ubomoaji wa nyumba zilizo maeneo hatarishi.
Wananchi pamoja na polisi (Wazee wa kazi) wakiangalia ubomoaji unavyoendelea bila vurugu.
Vijana wakiokota vitu mbalimbali katika maeneo yaliyobomolewa leo jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakiwa maeneo hatarishi ambayo yanasubiri kubomorewa.
Uondoaji wa vyuma katika nyumba inayongoja kubomolewa.
Vitu mbalimbali vikiwa vimetolewa nje ili kupisha ubomoaji wa nyumba.
hata ulaya kuna mabonde ila miundo mbinu ipo sawa, issue si kuwaacha wananchi wahangaike kama burundi, serikali inawasaidiaje hao? maana wanajuta kupiga kura, je shukrani ya kura ni kulala nje?
ReplyDelete