Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo nchini, Mhe. Juma - Alfani Mpango ambaye alikwenda ofisini
kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 2, 2015.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya kinyago Balozi wa Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo nchini, Mhe. Juma-Alfani Mpango ambaye
alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 2, 2015
kuaga.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo, Mhe. Juma- Alfani Mpango ambaye alikwenda ofisini kwa
Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 2, 2015 kuaga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
**********
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambaye anamaliza muda wake, Bw.
Juma-Alfani Mpango.
Akizungumza
na balozi Mpango leo (Jumatano, Desemba 2, 2015), ofisini kwake,
Magogoni jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu alimshukuru balozi huyo kwa
pongezi zake na kumuomba aendelee kuwa balozi mzuri wa kuitangaza
Tanzania hata baada ya kurejea nyumbani.
Pia
alitumia fursa hiyo kuwaombea heri wananchi wa DRC pamoja na Rais Joseph
Kabila katika maandalizi ya uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika
nchini humo mwakani.
Kwa
upande wake, Balozi Mpango ambaye alisema amekaa hapa nchini kwa miaka
12, alimweleza Waziri Mkuu kwamba amejifunza mengi sana kutoka kwa
viongozi wa Tanzania kubwa vikiwa ni uchapakazi na unyenyekevu. “Nimeona
utawala wa Rais Benjamin Mkapa, Rais Jakaya Kikwete na sasa Dkt. John
Pombe Magufuli. Ninavutiwa na hatua mnazochukua hivi sasa katika
kupambana na rushwa na ufisadi,” alisema.
“Mambo
niliyojifunza tangu nimekaa hapa ni uchapakazi na unyenyekevu. Unaona
kabisa kwamba mtu anaamini kuwa madaraka siyo kitu cha kujivunia kwa
mtumishi wa umma. Anachotakiwa kuwa nacho ni utayari wa kuwatumikia
wananchi,” alisema kwa Kiswahili sanifu.
Balozi
Mpango aliomba mahusiano ya nchi hizi mbili yaendelezwe kwani DRC
imekuwa ikinufaika na matumizi ya bandari ya Dar es Salaam katika
kusafirishia bidhaa zake kwenda nchi za nje.
“Bandari
ya Dar es Salaam ni muhimu sana kwetu. Mwaka 2004 tulisafirisha tani za
mizigo 200,000, mwaka 2014 ziliongezeka na kufikia tani milioni 1.3; na
mwakani tunataraji zitaongezeka na kufikia tani milioni tatu,” alisema.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATANO, DESEMBA 2, 2015.
0 comments:
Post a Comment