Nafasi Ya Matangazo

December 31, 2015


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman (aliyenyoosha mkono) akimpa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jingo la tatu la abiria, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Pro. Makame Mbarawa.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman (aliyenyoosha mkono) akimpa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jingo la tatu la abiria, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Pro. Makame Mbarawa.
Mhandisi Mohamed Millanga akiongoza msafara wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Prof. Makame Mbarawa kukagua ujenzi wa jengo la tatu la abiria (TBIII).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Prof. Makame Mbarawa (katikati) akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa TBIII kutoka kwa mhandisi Mohamed Millanga (kulia).
************
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh.Prof.  Makame Mbarawa ameagiza  watumishi wa Tassisi  zote  zinazotoa  huduma katika viwanja vya ndege  hapa nchini kuwajibika kwa Mameneja  wa Mamlaka  ya Viwanja vya Ndege  (TAA)  wanaosimamia  viwanja  ambavyo  watumishi hao wamepangiwa  kufanya  kazi.

Mh. Mbarawa ametoa agizo hilo jana wakati alipofanya ziara ya siku moja kwenye Makao Makuu  ya  TAA  ambapo  pamoja na mambo mengine  alikagua  ujenzi unaondelea wa jengo la tatu la abiria (TBIII), na  kituo cha Zimamoto na Uokoaji. Pia  alitembelea mradi  wa usimikaji wa vivuko vipya vya abiria (Passenger Boarding  Bridges) na  usimikaji wa mitambo mipya ya kufua umeme wa dharura (Standby Generators) iliyopo katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

Akizungumza  na menejimenti ya TAA ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi  Suleiman S. Suleiman  katika Ofisi  za TAA  ikiwa ni sehemu ya majumuisho ya ziara yake, Prof. Mbarawa aliwapongeza TAA kwa kazi nzuri wanayoifanya hususan  katika uboreshaji wa muindombinu na kuhudumia wateja. Hata hivyo alisema pamoja na sifa hiyo nzuri, kuna haja kwa TAA kuwa mdhibiti wa taasisi nyingine zote  zinazofanyakazi katika viwanja vya  ndege hapa nchini kama njia ya  kuepuka kuchafua sifa nzuri ya viwanja hivyo na nchi kwa ujumla.

“ Pamoja na kazi nzuri mnayoifanya,nadhani  wakati umefika sasa kwa taasisi zote zinazotoa huduma katika viwanja vya ndege hapa nchini  ziwe chini ya TAA”,  alisema  Prof. Mbarawa  huku akisisitiza umuhimu wa  taasisi hizo kufanya kazi  kwa kushirikiana  kama timu moja.  “Nyinyi ndio kioo katika jamii yetu, taasisi nyingine mfano uhamiaji wakachelewa kugonga mhuri kwenye hati za kusafiria, watu hawatambui kama ndio wao waliochelewesha na lawama watawatupia nyinyi,” alisisitiza Mh. Mbarawa na kuongeza kwamba anafanya utaratibu wa kuwasiliana na Wizara zote zinazohusiana  na taasisi hizo ili kupanga utaratibu muafaka.

Mbali na idara ya uhamiaji,  taasisi nyingine zinazotoa huduma kwenye viwanja vya ndege ni pamoja na Idara ya maliasili,  afya, kilimo, mifugo, madini,  polisi na kitengo cha kuzuia madawa ya kulevya. 

Mh. Mbarawa  pia  ameiagiza  TAA kubuni  mikakati  ya kuongeza ukusanyaji wa mapato zaidi ili iweze kujiendesha na pia ihakikishe kuwa inaepukana  na matumizi yasiyo ya lazima. Aliitaka watumishi wa TAA  kuzingatia uadilifu na weledi katika utendaji wao wa kazi na kuhudumia wateja  ikizingatiwa kuwa viwanja vya ndege ni kioo cha nchi.

“Nisingependa taarifa za matukio mbalimbali yanayotokea kwenye viwanja niyasikie au kuyaona kwenye vyombo vya habari wakati mimi mwenyewe sijui, hivyo tujenge utamaduni wa kuwa waadilifu na tufanye kazi kwa kuzingatia weledi, tuepukane na matukio ya hovyo,” alisisitiza Mh. Mbarawa.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi S.S.Suleiman alimhakikishia Waziri Mbarawa kutekeleza maagizo yake, likiwemo la kubuni mbinu mpya za mapato, na hata kuweka utaratibu wa kumpatia taarifa mbalimbali zinazotokea kwenye viwanja kabla hazijapelekwa sehemu nyingine yeyote, kwa ajili ya utekelezaji na kujenga uhusiano mzuri baina ya mamlaka na wizara kwa ujumla.

“Kuhusu mapato tunauhakika wakati wa jengo la tatu la abiria likifunguliwa yataongezeka, lakini tunaahidi kubuni mbinu nyingi zaidi, ili  tuwe na vyanzo vya uhakika vya mapato,” alisema Mhandishi Suleiman. Alisema kukamilika kwa jengo hilo kutaongeza idadi ya abiria watakaosafiri na ndege za ukubwa mbalimbali ikiwemo 380 Airbus yenye uwezo wa kubeba abiria 300.

Awali Mh. Mbarawa alipotembelea ofisi za zimamoto zilizopo JNIA, alielezwa wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa na hususan  magari ya zimamoto ambayo mbali na kuhudumia viwanja vya ndege, wakati mwingine  kulazimika pia kusaidia  jamii endapo nyumba zao zinakumbwa na majanga ya  moto.


       Imetolewa na kitengo cha Habari na Mahusiano na Sheria TAA.
Posted by MROKI On Thursday, December 31, 2015 No comments
Posted by MROKI On Thursday, December 31, 2015 No comments

 Msanii Tekno Miles (wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla iliyomtambulisha rasmi kwa waandishi wa habari iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Msanii huyo anatarajiwa kuburudisha katika Tamasha la mwisho la “Grown and Sexy, the Gold finale” litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga karibu na Best Bite katika mkesha wa mwaka mpya ambapo pia atafunga rasmi mfululizo wa matamasha hayo ya Grown And Sexy tokea kuanzishwa kwake.
Dj rasmi wa msanii Jay Z wa Marekani al maarufu kama “Young Guru” akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ya kumtambulisha rasmi Msanii Tekno Miles (Katikati) ambaye anatarajiwa kuburudisha katika Tamasha la mwisho la “Grown and Sexy, the Gold finale” litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga karibu na Best Bite katika mkesha wa mwaka mpya. Dj huyo atasimamia vilivyo kazi yake katika shughuli nzima ya Tamasha hilo. 
Meneja Chapa (pombe kali) wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija (Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Msanii Tekno Miles (wa kwanza kushoto) na Dj rasmi wa msanii Jay Z wa Marekani al maarufu kama “Young Guru” wakati wa hafla iliyomtambulisha Msanii Tekno Miles kwa waandishi wa habari iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Msanii huyo anatarajiwa kuburudisha katika Tamasha la mwisho la “Grown and Sexy, the Gold finale” litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga karibu na Best Bite katika mkesha wa mwaka mpya ambapo pia atafunga rasmi mfululizo wa matamasha hayo ya Grown And Sexy tokea kuanzishwa kwake.  SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Posted by MROKI On Thursday, December 31, 2015 No comments
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri akitoa ufafanuzi kwa Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kushoto) kuhusu utendaji wa Wakala hiyo leo wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Angella Kairuki katika Ofisi za Wakala hiyo leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Uratibu wa Miundombinu ya TEHAMA wa Wakala ya Serikali Mtandao Bw. Benjamin Dotto akitoa ufafanuzi kwa Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kulia) kuhusu kituo cha ufuatiliaji mifumo ya mawasiliano Serikalini leo jijini Dar es salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri akitoa ufafanuzi kwa Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kulia) kuhusu kituo cha ufuatiliaji mifumo ya mawasiliano Serikalini leo jijini Dar es salaam. 
Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kushoto) akipokewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri leo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala hiyo jijini Dar es salaam.
Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (katikati) akiwasili Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao kwa ziara ya kikazi leo jijini Dar es salaam.
Posted by MROKI On Thursday, December 31, 2015 No comments
1
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akiwasili Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC Upanga jijini Dar es salaam huku akilakiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Ndugu Nehemia Mchechu wakati waziri huyo akiwa katika ziara yake ya kujifunza na kusikiliza Changamoto na mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na shirika hilo.
2
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akiuliza jambo kwa mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba Bw. Nehemia Mchechu wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na shirika hilo.
3
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba Bw. Nehemia Mchechu wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na shirika hilo.
4
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akiwa katika kikao na wakuu wa vitengo mbalimbali wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na shirika hilo.
5
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano makao makuu ya NHC , kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba Bw. Nehemia Mchechu .
6
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano makao makuu ya NHC Upanga.
7
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hawapo pichani katika ukumbi wa mikutano makao makuu ya NHC Upanga.
8
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba Bw. Nehemia Mchechu akijibu baadhi ya maswali yalioulizwa na waandishi wa habari wakati Naibu Waziri Angelina Mabula alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea shirika hilo leo.
9
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba Bw. Nehemia Mchechu akijadiliana jambo na Muungano Saguya katikati na kulia ni Yahya Charahani Maafisa kutoka shirika hilo la NHC.
Posted by MROKI On Thursday, December 31, 2015 No comments
 Barabara zinazoingia katika Daraja la Kigamboni.
Mkurugezi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau akimkaribisha Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa alipofanya ziara ya kuangalia maendekleoa ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni.
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Karim Mattaka akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (kushoto), wakati alipofanya ziara kuangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo linalotarajiwa kuanza kutumiaka rasmi ifikapo Februari 2016. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau.
Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (kushoto), akizungumza wakati alipofanya ziara kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni ambalo linalotarajiwa kuanza kutumiaka rasmi ifikapo Februari 2016. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau.
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Karim Mattaka akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kulia) TAZAMA PICHA ZAIDI HAPA 
Posted by MROKI On Thursday, December 31, 2015 No comments
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako (kushoto), akisisitiza jambo, alipokuwa akizungumza na wafanykazi wa Baraza la Taifa la Elimu na Ufundi (NACTE) jana alipotembelea makao makuu ya baraza hilo lililopo jijini Dar es Salaam jana,wapili toka kushoto ni na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dk.Primus Nkwera.
Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako,akimsikiliza kwa makini Vincent Jacob, mtalamu wa mtandao wa udhibiti wa utoajia wa vyeti vya satifiketi na Diploma wa Baraza la Taifa la  Elimu na ufundi (NACTE). Waziri alifanya ziara ya kutembelea makao makuu ya baraza hilo jijini Dar es Salaam jana,Watatu kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dk.Primus Nkwera.
 Waziri wa Elimu Sayansi,Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kuzungumza na wafanyakazi wa Baraza la Taifa la  Elimu na ufundi (NACTE) jijini Dar es salaam jana.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa. Joyce Ndalichako, akitembezwa katika maeneo ya ofisi za Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) jijini Dar es salaam jana na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dk.Primus Nkwera. Waziri huyo alikuwa katika ziara ya kutembelea taasisi za elimu zilizochini ya wizara yake.
Posted by MROKI On Thursday, December 31, 2015 No comments
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dk. Ally Yahaya SIMBA

1.  Katika shughuili zake za udhibiti wa huduma za mawasiliano nchini, Mamlaka ya Mawasilaino Tanzania imepokea malalamiko kutoka kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano dhidi ya kuwepo mazingira yasiyo salama katika huduma za mawasiliano na hivyo kusababisha kufanyika kwa vitendo vya utapeli unaofanywa kwa kutuma jumbe za udanganyifu na kulaghai, hivyo kusababisha watu kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu. Kwa mfano kupokea ujumbe kutoka namba unayoifahamu ukikuagiza utume fedha au ujumbe wa kashfa au matusi wakati hautoki kwa mhusika mwenye namba. Mamlaka imepokea malalamiko mengi kutoka kwa wateja na malalamiko mengine hupelekwa Polisi. Kwa miezi miwili tu, matukio 42 yameripotiwa Polisi pamoja na TCRA ambayo tukio moja tu linakuwa na ulaghai wa takribani milioni 25 peke yake.

2.  Tarehe 16 Oktoba, 2015 Mamlaka iliwakumbusha watoa huduma za simu nchini juu ya wajibu wao kuchukua hatua za kusheria na kitaalamu ili kulinda watumiaji dhidi ya utumaji wa jumbe za kilaghai na kuchukua hatua mara moja kuzuia mitandao yao kutumika kutuma jumbe za udanganyifu na kulaghai. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Mamlaka tarehe 16 Desemba, 2015 Mamlaka ilibaini kuwa  kampuni za Benson Informatics Limited (inayojulikana kama Smart), MIC Tanzania Limited (inayojulikana kama Tigo), Airtel Tanzania Limited, Viettel Tanzania Limited (inayojulikana kama Halotel) and Zanzibar Telecom Limited inayojulikana kama Zantel) zimeshindwa, zimepuuzia na zimekataa kufuata maagizo ya Mamlaka kuchukua hatua mara moja kuzuia mitandao yao kutumika kutuma jumbe za kilaghai kinyume na Kanuni Na.8(a) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya mwaka 2011 [the Electronic and Postal Communications (Computer Emergency Response Team) Regulations, 2011].

3.      Tarehe 18 Disemba, 2015 Mamlaka iliwaamuru watoa huduma za mawasiliano waliotajwa hapo juu kufika mbele ya Mamlaka na kujieleza kwa nini hatua za kisheria zisichukuliwe dhidi yao kwa kuvunja sheria na kanuni ya 8(a) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielectroniki na Postal ya Mwaka 2011 [the Electronic and Postal Communications (Computer Emergency Response Team) Regulations, 2011] kwa kushindwa kuweka mazingira salama kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano.

4.      Watoa huduma walifika na kutoa maelezo ya utetezi kati ya tarehe 21 na 23 Desemba, 2015.

5.  Baada ya kuwasikiliza na kutilia maanani utetezi wa watoa huduma na kwa mujibu wa uchunguzi na majaribio uliofanywa na Mamlaka, Mamlaka imejiridhisha kuwa mitandao ya watoa huduma waliotajwa hapo juu haikuwa salama na kuwa watoa huduma hao walishindwa kufuata maelekezo ya Mamlaka juu ya kuweka mazingira salama katika huduma wanazotoa. Hivyo Mamlaka imejiridhisha kuwa watoa huduma wamekiuka matakwa ya Kanuni ya 8(a) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielectroniki na Postal ya mwaka 2011 (The Electronic and Postal Communications (Computer Emergency Response Team) Regulations, 2011) inayowataka watoa huduma kuweka mazingira ya mitandao salama kwa kuchukua hatua za kusheria na kitaalamu ili kulinda watumiaji dhidi ya uhalifu ikiwa ni pamoja na utumaji wa jumbe za kilaghai kupitia mitandao yao.

6.  Kwa mujibu wa Kifungu cha 17 cha Jedwali la Pili katika Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, Sura ya 306 ya Sheria za Nchi, kinachoipa Mamlaka uwezo wa kutoa adhabu kwa Wenye Leseni dhidi ya uvunjifu wa Sheria, Kanuni na Masharti ya Leseni, Mamlaka ya Mawasiliano imetoa:

A.          Onyo kali kwa Kampuni za:
(i)           Benson Informatics Limited (inayojulikana kama Smart),
(ii)           MIC Tanzania Limited (inayojulikana kama Tigo),
(iii)          Airtel Tanzania Limited,
(iv)          Viettel Tanzania Limited (inayojulikana kama Halotel), na
(v)          Zanzibar Telecom Limited (inayojulikana kama Zantel).

kwa kushindwa kutimiza matakwa ya Kanuni ya 8(a) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Postal ya mwaka 2011  [the Electronic and Postal Communications (Computer Emergency Response Team) Regulations, 2011] kwa kushindwa kuweza mazingira salama kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano.

B.          Imeamuru Kila Kampuni husika:
(i)       Kuhakikisha kuwa, kuanzia siku ya kutolewa kwa amri hii, inaweka mazingira salama katika mtandao wake yatakayozuia utumaji wa jumbe za kilaghai (yaani ‘spoofed messages’) na matishio mengine ya kiusalama;
(ii)      Kulipa faini ya Shilingi za Kitanzania Milioni Ishirini na Tano (Shs 25,000,000.00) kwa Mamlaka ya Mawasiliano kabla ya tarehe 29 Januari, 2016; na
(iii)   Endapo Makamuni haya yatashindwa kutimiza amri Na.2 hapo juu, Mamlaka itachukua hatua zaidi za kisheria na kiudhibiti dhidi ya Kampuni ya Simu husika.

7.      Aidha, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inapeda kuchukua fursa hii kuwatahadharisha wananchi kuwa makini na jumbe za kuwataka kutuma fedha bila ya kuwa na uhakika. Inashauriwa kuhakiki ujumbe husika kwa kupiga simu na kuongea na mhusika kabla ya kufanya maamuzi ya kutuma fedha hata kama namba inayotumika unaijua. Vilevile wawe makini wanapopokea jumbe zinazoonesha zinatoka kwa mtu fulani wanayemjua kumbe ni matapeli wanaotumia ulaghai kwa njia hii ya “spoofing”.

IMETOLEWA NA

………………………………………….
Dkt. Ally Y. Simba
MKURUGENZI MKUU

30 Disemba, 2015
Posted by MROKI On Thursday, December 31, 2015 No comments
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa makatibu wakuu na manaibu Katibu wakuu katika Wizara mbalimbali.

Walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
  1. Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi - Ombeni Sefue
  1. Katibu Mkuu Ikulu
Peter Ilomo
  1. Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
Dkt. Laurian Ndumbaro
  1. Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhandisi Mussa Iyombe (Katibu Mkuu)
Dkt. Deo  Mtasiwa (Naibu Katibu Mkuu - Afya)
Bernard Makali (Naibu Katibu Mkuu - Elimu)
  1. Ofisi ya Makamu wa Rais
            Mbaraka A. Wakili ( Katibu Mkuu)
            Mhandisi Ngosi Mwihava (Naibu Katibu Mkuu)

  1. Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Sera, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu)
Erick Shitindi (Katibu Mkuu Kazi na Ajira)
Mussa Uledi (Katibu Mkuu Bunge)
Dkt. Hamis Mwinyimvua (Katibu Mkuu - Sera)

  1. Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Dkt. Frolence Turuka (Katibu Mkuu - Kilimo)
Dkt. Mashingo (Katibu Mkuu Mifugo)
Dkt. Budeba (Katibu Mkuu - Uvuvi)

  1. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi Joseph. Nyamuhanga (Katibu Mkuu - Ujenzi)
Dkt. Leonard M. Chamuliho (Katibu Mkuu - Uchukuzi)
Profesa Faustine R. Kamuzora (Katibu Mkuu - Mawasiliano)
Mary Sassabo (Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano)

  1. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Dkt. Yamungu Kayandabira (Katibu Mkuu)
Dkt. Moses Kusiluka (Naibu Katibu Mkuu)
  1. Wizara ya Maliasili na Utalii
Meja Jenerali Gaudence S. Milanzi (Katibu Mkuu)
Anjelina Madete (Naibu Katibu Mkuu)
  1. Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
Dkt. Adelhem James Meru (Katibu Mkuu - Viwanda)
Profesa Adolf F. Mkenda (Katibu Mkuu - Biashara na Uwekezaji)
Mhandisi Joel Malongo (Naibu Katibu Mkuu)

  1. Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
Maimuna Tarishi (Katibu Mkuu)
Profesa Simon S. Msanjila (Naibu Katibu Mkuu)
Dkt. Leonard Akwilapo (Naibu Katibu Mkuu)
  1. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dkt. Mpoki Ulisubisya (Katibu Mkuu - Afya)
Sihaba Nkinga (Katibu Mkuu - Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto)
  1.  Wizara ya Habari, Utamaduni,  Sanaa na Michezo
Profesa Elisante Ole Gabriel Mollel (Katibu Mkuu)
Nuru Halfan Mrisho (Naibu Katibu Mkuu)
  1. Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Mhandisi Mbogo Futakamba (Katibu Mkuu)
Mhandisi Kalobero Emmanuel (Naibu Katibu Mkuu)
  1.  Wizara ya Nishati na Madini
Profesa Justus W. Ntalikwa (Katibu Mkuu)
Profesa James Epifani Mdoe (Naibu Katibu Mkuu)
Dkt. Paulina Pallangyo (Naibu Katibu Mkuu)
  1.  Wizara ya Katiba na Sheria
Profesa Sifuni Mchome (Katibu Mkuu)
Suzan Paul Mlawi (Naibu Katibu Mkuu)
Amon Mpanju (Naibu Katibu Mkuu)
  1.  Wizara ya Mambo ya Ndani
Jaji Meja Jenerali Projest A. Rwegasira (Katibu Mkuu)
Balozi Hassan Simba Yahaya (Naibu Katibu Mkuu)

  1.  Wizara ya Fedha na Mipango
Dkt. Silvacius Likwelile (Katibu Mkuu)
Dorothy Mwanyika (Naibu Katibu Mkuu)
James Dotto (Naibu Katibu Mkuu)
Amina Hamis Shaban (Naibu Katibu Mkuu)
  1. Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Dkt. Aziz Mlima (Katibu Mkuu)
Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi ( Naibu Katibu Mkuu)
  1. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Job D. Masima (Katibu Mkuu)
Immaculate Peter Ngwale (Naibu Katibu Mkuu

Makatibu wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wote ambao hawajatajwa katika orodha hii watapangiwa kazi nyingine.

Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Eliakimu Maswi kuwa Kaimu Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na ametengua uteuzi wa Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Lusekelo Mwaseba, ambaye atapangiwa kazi nyingine

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

30 Desemba, 2015
Posted by MROKI On Thursday, December 31, 2015 No comments
Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (katikati) akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kuwatafuta washindi wa droo ya nne ya promosheni ya "Jaza Mafuta na Ushinde" inayowawezesha wateja wake kujipatia lita 40 za mafuta kwa kila mshindi wa droo hiyo kila wiki. Kulia ni Mkaguzi wa michezo ya kubahatisha nchini, Bakari Maggid, na kushoto ni Meneja wa Fedha wa Kampuni ya mafuta ya GAPCO Tanzania, Michael Chobu.
Posted by MROKI On Thursday, December 31, 2015 No comments

December 29, 2015

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa akizungumza na uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), wakati alipotembelea bandarini hapo leo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa akiongozana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Eng. Edwin Ngonyani pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa Iyombe wametembelea Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kwa mara ya pili tangu alipoapishwa jana.

Aidha Waziri Mbarawa katika ziara yake hiyo ametembelea pia na Shirika la Reli Tanzania (TRL), na kupokea taarifa ya utendaji wa kazi wa taasisi hizo kama picha zinavyoonesha:
 Maafisa wa Wizara na Watendaji wa Mamlaka ya Bandari wakimsikiliza kwa makini Mhe. Waziri Mbarawa alipokuwa akitoa maelekezo ya kazi katika ofisi za Meneja wa Bandari mkoa wa Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa (kushoto) na Naibu wa Wizara hiyo Eng. Edwin Ngonyani (kulia) wakipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Eng. Mshana (katikati) mara walipowasili kwenye ofisi za Shirika hilo.
 Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa Iyombe akifafanua jambo wakati wa upokeaji wa taarifa ya utendaji kazi wa TRL.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Eng. Mshana (wa kwanza kushoto), akitoa taarifa ya changamoto zinazoikabili shirika hilo kwa Mhe. Waziri Mbarawa.
Waziri Mbarawa akisisitiza jambo alipokuwa akitoa maelekezo kwa watendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), jijini Dar es Salaam.
Posted by MROKI On Tuesday, December 29, 2015 No comments
zit2
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua dagaa wanaokaushwa kitalaam kwa kutumia jua  wakati  alipozindua soko na mwaro wa kisasa wa samaki wa Kibirizi  mjini Kigoma Desemba 28, 2015. zit1
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizindua soko na Mwaro wa samaki wa Kibirizi mjini Kigoma Desemba 28 , 2015.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo Issa Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizindua soko na Mwaro wa samaki wa Kibirizi mjini Kigoma Desemba 28 , 2015.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo Issa Machibya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Machibya.
zit5
Mkazi wa Kigoma mjini akionyesha bango katika mkutano uliohutubiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye soko la samaki la Kibirizi mjini Kigoma Desemba 28, 2015.
zit6
Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Kigoma, Issa Machibya kuhusu bunduki iliyokatwa ili kupunguzwa urefu ambayo ilikamatwa na polisi mkoani Kigoma wakati ilipotumika katika uhalifu. Mheshimiwa Majaliwa alikwenda kwenye Ofisi ya  Kamanda  wa polisi wa Mkoa wa Kigoma kukagua silaha mbalimbali zilizokamatwa na polisi  Desemba 28, 2015.
zit7
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa  akitazama kifaa kinachotumiwa na wahalifu kutengeneza  risasi za bunduki aina ya goboli wakati alipokagua silaha mbalimbali zilizokamatwa na polisi  mkoani Kigoma na kuhifadhiwa kwenye Ofisi ya Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Desemba 28, 2015. 
zit8
 Watumishi wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa  wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majliwa  wakati alipowahutubia  mjini Kigoma Desemba 28, 2015. 
zit9
 Watumishi wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa  wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majliwa  wakati alipowahutubia  mjini Kigoma Desemba 28, 2015. 
zit10

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa  akizungumza na watumishi wa  serikari Kuu na Serikali za Mitaa mjini Kigoma Desema 28, 2015. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Posted by MROKI On Tuesday, December 29, 2015 No comments
  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo