Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa akizungumza na
uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), wakati alipotembelea bandarini hapo
leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa akiongozana na
Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Eng. Edwin Ngonyani pamoja na aliyekuwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa Iyombe wametembelea Mamlaka ya Bandari
Tanzania (TPA), kwa mara ya pili tangu alipoapishwa jana.
Aidha
Waziri Mbarawa katika ziara yake hiyo ametembelea pia na Shirika la Reli
Tanzania (TRL), na kupokea taarifa ya utendaji wa kazi wa taasisi hizo kama
picha zinavyoonesha:
Maafisa wa Wizara na Watendaji wa Mamlaka ya Bandari
wakimsikiliza kwa makini Mhe. Waziri Mbarawa alipokuwa akitoa maelekezo ya kazi
katika ofisi za Meneja wa Bandari mkoa wa Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof.
Makame Mbarawa (kushoto) na Naibu wa Wizara hiyo Eng. Edwin Ngonyani (kulia)
wakipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania
(TRL), Eng. Mshana (katikati) mara walipowasili kwenye ofisi za Shirika hilo.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa
Iyombe akifafanua jambo wakati wa upokeaji wa taarifa ya utendaji kazi wa TRL.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Eng. Mshana (wa kwanza kushoto), akitoa taarifa ya changamoto zinazoikabili shirika hilo kwa Mhe. Waziri Mbarawa.
Waziri Mbarawa akisisitiza jambo alipokuwa akitoa
maelekezo kwa watendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), jijini Dar es
Salaam.
0 comments:
Post a Comment