Nafasi Ya Matangazo

November 07, 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.  Servacius Likwelile alipotembelea ofisi za Wizara ya Fedha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipata ufafanuzi kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.  Servacius Likwelile wakati wa ziara hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na uongozi wa Wizara ya Fedha.
***************
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika Ofisi za Wizara ya Fedha leo Ijumaa tarehe 6 Novemba, 2015.

Katika ziara hiyo Mhe.Rais alipata fursa ya kutembelea baadhi ya Ofisi za Wizara na baadae  kuzungumza na Viongozi wa Wizara ili kufahamu changamoto ambazo zinaikabili Wizara ya Fedha.

Wakati akimkaribisha Mhe.Rais Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha        Dkt. Servacius Likwelile alimueleza kuwa Wizara ya Fedha inakabiliwa na changamoto kubwa inayotokana na makusanyo ya mapato ya ndani.  Miongoni mwa sababu ni misamaha ya kodi, wafanyabiashara wengi hasa wakubwa kukwepa kodi, makusanyo yasiyoridhisha ya maduhuli na kutokulipwa kwa kodi za majengo. Aidha Dkt. Likwelile alishauri ni bora kuwekwa mifumo mizuri, ikiwemo matumizi ya Tehama na EFDs. 

“Pamoja na ziara yangu kuwa ni ya kustukiza nimefurahi sana kukuta Viongozi wote wapo ofisini na wanafanya kazi. Jambo hili limenipa faraja kubwa. Ziara yangu ya kuja hapa nimejifunza na kujua changamoto zipi zinazowakabili”. Alisema Mhe. Rais.

Nimesikia changomoto nyingi na ninaagiza kuwa muhakikishe walipa kodi wakubwa wanalipa kodi na kusimamia kikamilifu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili iweze kukusanya kodi kikamilifu na si kuwabana wafanya biashara wadogo wadogo.

Mhe.Rais aliwataka Viongozi wa Wizara kufanya kazi kwa bidii ili kuvuka lengo.

Imetolewa na;
Msemaji wa Wizara ya Fedha
Ingiahedi C.Mduma
6.11.2015      
Posted by MROKI On Saturday, November 07, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo