Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru akizungumza na Waandishi wa Habari (hawako pichani) leo tarehe 23/11/2015 katika Ofisi za Wizara hiyo ambapo amesema kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imechaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Urithi wa Dunia kwa kipindi cha miaka minne. Uchaguzi huo umefuatia uamuzi wa Mkutano Mkuu wa 20 wa nchi Wanachama wa Mkataba wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) unaohusu Urithi wa Dunia uliofanyika mjini Paris, Ufaransa tarehe 18-20 Novemba 2015.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru kushoto akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Tanzania kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Urithi wa Dunia. Alieleza kuwa katika Kamati hiyo Tanzania itawakilishwa na Bw. Donatius Makamba ambaye ni Mkurugugenzi Idara ya Mambo ya Kale Wizara ya Maliasili na Utalii akisaidiwa na Dkt. James Wakibara, Mwikolojia Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA) na Dkt. Mohammed Juma, Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji kutoka Zanzibar.
Bi. Eliwasa Maro Mkurugenzi Msaidizi Utafiti Mafunzo na Takwimu Wizara ya Maliasili na Utalii akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo katika Mkutano huo na Waandishi wa Habari.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano huo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wakinukuu baadhi ya mambo muhimu.
0 comments:
Post a Comment