Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mifuko ya Hifadhi
ya Jamii, SSRA, Omar Kahlfan, (atikati), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSPF,
Neema Muro, (wapili kushoto), Meenja wa Mpango wa Uchagiaji wa Hiari wa
PSPF,Mwanjaa Sembe, (wakwanza kushoto) na maafisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya, NHIF, (kulia walosimama), wakishuhudia Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam
Mayinhu, (kushoto) na Kaimu MkurugeNzi Mkuu wa NHIF, Michael Mhando, wakitia
saini makubaliano ambayo yatawezesha taasisi hizo mbili kushirikiana ambapo
Wanachama wa PSPF wa Uchangiaji wa Hiari, watadhaminiwa na Mfuko huo ili waweze
kuingizwa kwenye utaratibu wa kupatia bima ya afya kutoka NHIF. Makubaliano
hayo yaklifikiwa leo Jumatano Novemba 18, 2015 makao makuu ya PSPF jijini Dar
es Salaam.
Bw. Mayingu, (kushoto) na Bw. Mhando wakibadilishana hati baada ya kuzisaini
************
Na K-Vis Media/Khalfan Said
MFUKO wa Pensheni wa PSPF, na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF,
wameingia makubaliano yatakayowezesha wanachama wa PSPF, kupitia mpango wa
Uchangiaji wa Hiari yaani PSS, kuanza kupata matibabu kwenye hospitali zote
zenye mkataba na NHIF.
Makubaliano hayo yametiwa saini leo Jumatano Novemba 18, 2015, kati ya
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,
Bw.Michael C.t.M Mhando na kufuatiwa na uzinduzi rasmi ambapo wanachama wa
kwanza zaidi ya 10 wamepatiwa kadi za Bima ya Afya.
Hafla hiyo ilifanyika makuu ya PSPF, jingo la Jubilee Towers jijini Dar
es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Mayingu
alisema, uamuzi huo wa PSPF kushirikiana na NHIF, ni utekelezaji wa malengo na
ahadiz a serikali ya awamu ya tano chini ya Rais, Dtk. John Pombe Magufuli,
ambaye aliwaahidi Watanzania wote wanapata huduma za afya zilzio bora. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA.
“ Katika kuhakikisha ahadi
hiyo ya Mheshimiwa Rais inatimizwa PSPF kwakushirikiana na wenzetu wa Mfuko
waTaifa wa Bima ya Afya tutatoa huduma za afya kwa wanachama wa Mpango wa
Uchangaji wa Hiari wa PSPF.” Alsiema Bw. Mayingu katika hotuba yake. Naye Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Michael Mhando alisema, wakati PSPF wamebobea
katika suala la pesheni, NHIF wao wamebobea katika kutoa huduma za afya, hivyo
ushirikiano wa Taasisi hizi mbili zenye uzoefu wa kuhudumia maisha ya
Watanzania, utakuwa umewapa unafuu mkubwa wa maisha. wajasiriamali wadogo ambao
kwa kuwekeza katika afya kutawawezesha ushiriki kikamilifu katika shughuli za
ujenzi wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Michael Mhando, (wapili kulia), wakizindua mpango huo huku Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Omar Khalfan akishuhudia
Bw. Mayingu akitoa hotuba yake
Bw. Mhando hotuba yake
Maafisa kutoka NHIF
Mwanachama wa PSPF, akisoma vipeperushi, vyenye maelezo na huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo
Mmoja wa waandishi wa habari akijaza fomu za kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari PSS
Kaimu Murugenzi Mtendajiw a NHIF, Bw. Michael Mhando (kushoto), akifurahia jambo na Meneja Uendeshaji wa PSPF, Bi. Neema Muro
Mwanachama wa mpango wa Uchagiaji wa Hiari PSS, akipokea kadi ya bima ya Afya, kutoka kwa mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Omra Khalfan (kulia)
Mwanachama wa SPF, Constantine Edward (kushoto) akipokea kadi yake
Meneja Msoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Costantina Martin,akitoa maelezowakati wa hafla hiyo
Meneja wa Mpango wa Uchangiajiwa Hiari, PSS, wa Mfuko wa Penshni wa PSPF, Bi.Mwanjaa Sembe, (wakwanza kulia), na afisa wa PSPF, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafaidika wakwanza wa mpango wa Mfuko huo kuwapatia matibabu wanachma wake wa mpango wa PSS
Mzee Mohammed Madenge, watatu kushoto), ambaye ni Mwanachama wa PSPF, wakwanza kufaidika na mpango wa bima ya afya, akitoa neon la shkrani kwa niaba ya wenzake
0 comments:
Post a Comment