Nafasi Ya Matangazo

November 18, 2015



Mrembo wa Taifa Miss Tanzania Lilian Deus Kamazima atakabidhiwa Bendera ya Taifa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck sadiq ikiwa ni ishara ya kumtakia kila la heri katika mashindano ya urembo ya Dunia yatakayofanyika Sanya China tarehe 19 Desemba 2015.


Mrembo huyo ataondoka nchini Ijumaa ya tarehe 20 Novemba 2015 na ataungana na waremboe wengine kutoka nchi zaidi ya 120 duniani  na watapiga kambi ya mwezi mmoja katika Hotel ya Beuaty Crown Sanya China.


Miss Tanzania Lilian amekuwa katika maandalizi ya kutosha tangu achukue Taji hilo mwezi Oktoba 2014

Pamoja na mambo mengine ameshiriki  Onyesho la Mavazi la nchi za Afrika ya Mashariki lililoandaliwa na Kampuni ya Arapapa Fashion ya mjini Kampala Uganda mwezi Novemba 2014.


Ameshiriki katika shughuli mbalimbali za Jamii katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na D’salaam.

Kama Balozi wa Hospital ya CCBRT Miss Tanzania Lilian anaondoka na ujumbe wa kupiga vita na kupambana na matatizo ya wasichana na akina mama ya Fistula.

Liliana alivikwa taji hilo la Miss Tanzania baada ya mrembo aliyetwaa taji hilo awali Siti Mtevu kuvuliwa kutokana na mapungufu yaliyojitokeza hadi kushinda taji hilo.  

Nancy Sumari ndiye mrembo pekee wa Tanzania aliyeshiriki mashindano ya dunia mwaka 2005 na kufanikiwa kutwaa taji la Miss World Afrika
Posted by MROKI On Wednesday, November 18, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo