Mbunifu
wa Mavazi nchini, Mustafa Hassanali akizungumza na Waandishi wa Habari
hawapo pichani juu ya umuhimu wa Amani hususani katika kuelekea
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, Mwaka huu na kusisitiza onyesho la mavazi
litakalo fanyika tarehe Oktoba 17 Mwaka huu katika ukumbi wa King
Solomon uliopo Eater Point Namanga, ambalo litakaloonyesha kazi za wa
wabunifu mbalimbali kama Kiki Zimba pamoja na Martin Kadinda.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari wakisikiliza kwa makini taarifa iliyokuwa
inatolewa na Mbunifu Mkongwe wa Mavazi Barani Afrika,Mstafa Hassanali
juu ya umuhimu wa Amani hususan kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Octoba
25,Mwaka huu.
*****************
Na Bakari Issa
Wabunifu wa Mavazi nchini Tanzania, Mustafa Hassanali,Kiki
Zimba pamoja na Martin Kadinda wameazimia kukusanya nguvu kwa pamoja ili
kuhubiri juu ya umuhimu wa Amani hususan kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Octoba
25,Mwaka huu.
Wabunifu hao wamekusanya nguvu kwa pamoja kwa kuwa na
onyesho la mavazi litakalo fanyika tarehe 17 Octoba Mwaka huu katika ukumbi wa
King Solomon uliopo Eater Point Namanga,ambalo litakalo onyesha kazi za ubunifu
zilizofanywa na wabunifu hao watatu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es
Saalam,Mbunifu Mkongwe wa Mavazi Barani Afrika ,Mustafa Hassanali amesema
kutokana na wimbo wetu wa Taifa “Hekima,Umoja na Amani,hizi ni Ngao zetu”kuna
umuhimu kwa vijana kukuza na kulinda Uhuru,Amani na Utulivu wa nchi.
Kwa Upande wake,Martin Kadinda amesema Uchaguzi Mkuu ni wa
muhimu sana,hivyo basi vijana wa Kitanzania wahakikishe wanapiga kura kwa Amani
katika Uchaguzi Mkuu wa Octoba 25 na kukaa katikahali ya Utulivu kwa kufuatilia
na kukubali matokeo yatakayotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) katika
hali ya Amani.
0 comments:
Post a Comment