Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania wakishindana kucheza muziki chini ya bomba la mvua wakati wa bonanza la siku ya familia ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania wakifurahia michezo katika bwawa la kuogelea la Hoteli ya Kunduchi Beach Wet in Wild, katika siku ya familia wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania wakifurahia michezo ya bembea hafla ya siku ya familia ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya wafanyakazi na wanafamilia wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania wakianza mashindano ya mbio za magari madogo yaendayo kasi ‘Go Kat’ katika maadhimisho ya siku ya wanafamilia hao jijini Dar es Salaam jana. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Wafanyakazi na familia zao wakichukua chakula kwa pamoja kuonyesha
upendo na mshikamano wao ambao pia ni sehemu ya mambo muhimu yanayochangia mafanikio kampuni yao.
Mmoja wa watoto wa wafanyakazi wa Airtel akimpakulia mwenzake kama ishara ya upendo wakati wa siku ya wanafamilia wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kulia), akibadilishana mawazo na baadhi ya wa wafanyakazi wa kapuni hiyo katika maadhimisho ya siku ya wanafamilia wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
Tanzania, Patrick Foya (kushoto) akimpomgeza Hagulwa Joseph, mtoto aliyeshinda katika shindano la kusakata dansi lililofanyika kunogesha bonanza la siku ya familia ya kampuni hiyo jijini Dar es Saalaam jana.
****************
WITO umetolewa kwa wafanyakazi nchini kushiriki michezo kwani kwa kufanya hivyo kutaweza kuimairisha afya zao hivyo kuongeza ufanisi mahali pao pa kazi.
Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam na Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu za Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania, Jane Matinde wakati wa bonanza la kila mwaka la siku ya wanafamilia wa kampuni hiyo.
Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam na Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu za Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania, Jane Matinde wakati wa bonanza la kila mwaka la siku ya wanafamilia wa kampuni hiyo.
Bi Jane alisema michezo ni kichocheo muhimu katika afya ya mwili na akili hivyo endapo wafanyakazi watashiriki katika shughuli za michezo kutaifanya miili yao isiwe goigoi.
"Moja ya mambo muhimu katika maendeleo mahali pa kazi ni bila shaka ni kuwa na wafanyakazi wenye afya ya mwili na akili, sisi kama Airtel Tanzania tunajali sana afya za wafanyakazi wetu," alisema.
Naye Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Airtel Tanzania, Patrick Foya alisema ni desturi yao kuwa na siku maalumu kila mwaka ya kuwakutanisha wafanyakazi wao na familia zao ili pamoja na kushiriki michezo na mambo mengine ya kuburudisha nyoyo zao zao lakini pia huitumia siku hiyo kuzidi kuimarisha mshikamano miongoni mwao.
"Umoja na mshikamano ni nyenzo muhimu mahali pa kazi, lakini pia ukiwa na mfanyakazi anayetoka katika familia iliyokosa utulivu, lakini pia mfanyakazi legelege hawezi kufanya kazi zake kwa ufanisi," akaongeza Bwana Foya.
Zaidi ya wafanyakazi na wanafamilia za 500 walishiriki katika bonanza hilo na kushiriki michezo mbalimbali kama vile kucheza muziki, kuvutaka kamba, soka la baharini, wavu na kuogelea.
0 comments:
Post a Comment