Mshambuliaji wa timu ya Simba, Hamisi Kiiza ndiye mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Septemba.
Kwa kuibuka mchezaji bora, Kiiza atazawadiwa sh. milioni moja kutoka kwa mdhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom.
Kiiza ambaye ameisadia Simba kufanya vizuri kwenye mwezi huo, ikiwemo
kufunga mabao matatu (hat trick) kwenye mechi dhidi ya Kagera Sugar
aliwashinda washambuliaji wa timu za Stand United (Elias Maguli) na
Yanga (Amisi Tambwe).
Ndani ya mwezi Septemba ambapo zilichezwa raundi tano, Kiiza amefunga jumla ya mabao matano.
LIGI KUU YA VODACOM KUENDELEA WIKI HII
Ligi kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho
Jumatano kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja tofauti nchini, huku
timu 8 zikisaka kupata pointi tatu muhimu.
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Young Africans watawakaribisha
Toto Africans, mchezo utakaonza majira ya saa 10:30 jioni, mjini
Shinyanga Stand United watakua wenyeji wa Majimaji katika uwanja wa
Kambarage mjini humo.
Tanzania Prisons watawakaribisha Simba SC katika uwanja wa Sokoine
jijini Mbeya, huku Wagosi wa Kaya, Coastal Union wakiwakaribisha Kagera
Sugar katika uwanja wa Mkwakani jijini Tanga.
Alhamis ligi hiyo itanendelea kwa michezo minne pia kucheza katika
viwanja mbalimbali, JKT Ruvu wataikaribisha Mtibwa Sugar uwanaj wa
Karume jijini Dar es salaam, Mwadui FC watacheza dhidi ya Mgambo
Shooting katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga.
Jijini Mbeya, Mbeya City watawakaribisha African Sports katika uwanja
wa Sokoine, huku Ndanda FC wakiwa wenyeji wa waoka mikate wa bakhresa
Azam FC katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
0 comments:
Post a Comment