Nafasi Ya Matangazo

October 20, 2015

Mwamndishi wa Habari na Blogger, Mroki Mroki 'Father Kidevu' pichani, ameishushia sifa simu mpya ya kisasa ya Huawei P8 kutokana na ubora wake wa kufanya kazi.

Akizungumza wakati wa kutafuta maoni juu ya simu hiyo, Father Kidevu amesema hivi sasa kama blogger ameweza kufanya kazi zake za blog bila hata ya kuwa na 'Laptop' na kazi ambayo anaweza ifanya mahali popote.

"Nimetumia simu aina nyingi, lakini hii Huawei P8 ni burudani, sasa hivi naweza kupiga picha za tukio lolote na kuipandisha katikia katika blog yangu bila shida hasa ukizingatia uwezo wa simu hii na wepesi wa kufungua mtandao", alisema Kidevu.

Aliongeza kuwa "Simu hii inauwezo mkubwa sana hasa ubora wa picha zake za mnato na video na hata unasaji wa sauti ulio katika ubora wa hali ya juu.".
Father Kidevu akiperuzi katika mtabndao kupitia simu yake ya Huawei P8.
Posted by MROKI On Tuesday, October 20, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo